Mbunge mmoja nchini Kenya ameshtakiwa kwa kughushi vyeti vya masomo yake, mwendesha mashtaka wa umma alitangaza jana Jumatano.
George Koimburi, Mbunge wa eneo bunge la Juja, anakabiliwa na mashtaka sita-matatu kwa madai ya kughushi nyaraka za masomo na tatu kwa kuwasilisha kama halisi.
Alikana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu.
Waendesha mashtaka wanadai Koimburi alighushi cheti chake cha shule ya upili na vyeti viwili vya kushiriki kozi ya chuo kikuu. Chini ya sheria za Kenya, wagombea ubunge lazima wawe wamemaliza shule ya upili.
Visa vya wanasiasa kuwasilisha vyeti ghushi vya kitaaluma si vya kawaida nchini Kenya, ingawa kufunguliwa mashitaka kwa mafanikio bado ni nadra.