Hamas itawaachilia mateka sita walio hai wa Israel siku ya Jumamosi, na kuongeza maradufu idadi iliyopangwa awali.
Hawa ndio mateka walio hai wa mwisho waliowekwa kuachiliwa chini ya awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano ulioanza Januari.
Wanamgambo hao wameripotiwa kuongeza idadi hiyo baada ya Israel kuruhusu nyumba zinazohamishika na vifaa vya ujenzi katika Ukanda wa Gaza ulioharibiwa.
Mateka hao wanatarajiwa kuachiliwa ili kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel.
Pande zinazozozana bado hazijajadili awamu ya pili, yenye changamoto zaidi ya kusitisha mapigano.