Walanguzi wa mazao ya wakulima wa kahawa, mahindi, mbogamboga na karanga wameondoka baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Ilolo-Ndolezi yenye urefu wa Km 11.01 kwa kiwango cha lami katika
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Isiniza kijiji cha Mbimba wamesema kuwa barabara hiyo imewarahisishia kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi kwenye masoko, hivyo kuwaongezea kipato.
Bi. Salome Nzunda amesema wanaishukuru serikali kwa kuwajengea barabara hiyo ambapo zamani ilikuwa na changamoto sana kwani barabara haikuwa inapitika.
“Zamani tulikuwa tunapita barabara ya kutoka Vwawa kwenda Ndolezi, ilikuwa na changamoto sana hata mtu akiumwa kwenda hospitali ya wilaya ilikuwa kazi, barabara ilikuwa haipitiki hata vifo vya wajawazito na watoto vilikuwepo sana”
“Tulikuwa tunashindwa kupita kwenye barabara hii, ilikuwa tope haswa na tulikuwa tukitumia hadi saa mbili kwenda mjini, lakini sasa hivi tunatumia dakika 15 kufika mjini, tunaishukuru serikali wametutengenezea barabara hii tunaweza kufika hospitali ya wilaya hata ya mkoa na vifo sasa hivi vimepungua”, aliongeza.
Kaimu Meneja wa TARURA mkoa wa Songwe, Mhandisi Lugano Mwambingu amesema barabara ya Ilolo-Ndolezi imejengwa kupitia mradi wa Agri-Connect kwa thamani ya Shilingi Bilioni 6.46 na hadi sasa umekamilika kwa 100%.
Amesema barabara hiyo imejengwa kwa kiwango cha lami pia wamejenga safu za boksi kalavati (3), safu za zege 35 kuweka alama za barabarani 50, mfereji wa maji ya mvua Km 6.456 pamoja na kuweka taa za barabarani 40.
Aidha, Mhandisi Mwambingu ameongeza kusema kwamba barabara hiyo imesaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara pamoja na mpango wa kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wanaoishi katika Kata za Iyula, Idiwili na Mlangali.
“Barabara hii imekuwa na muhimu sana kwa wakulima wa vijiji hivi kwani imefungua fursa za kiuchumi katika bonde hilo kwani kila zao linakubali na kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja.