Gordon Cordeiro ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 1994 kwa mauaji aliyoyakana vikali hatimaye ameachiwa huru baada ya miaka 30 gerezani ambapo uamuzi huo umetolewa baada ya ushahidi mpya wa DNA kuthibitisha kuwa hakuwa mhusika wa uhalifu huo.
Mara baada ya kutoka Gerezani kituo chake cha kwanza kilikuwa kaburi la mama yake huko Hawaii akimshukuru kwa kumlinda katika kipindi chote cha mateso yake na katika mahojiano yake ya kwanza akiwa Mtu huru Cordeiro alieleza mshtuko wa mabadiliko aliyoyakuta nje ya Gereza akisema kuwa dunia imebadilika sana, hasa kwa jinsi Watu walivyozama katika simu zao.
“Shukrani kwa DNA mpya,” alisema kwa tabasamu akitambua nguvu ya teknolojia katika kuthibitisha ukweli.
Ingawa ameachiwa huru Ofisi ya Mwendesha mashtaka inapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, lakini kwa uoande wake Cordeiro yeye anapanga kutumia muda wake kusaidia Familia na labda kurudisha fadhila kwa jamii.