Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania [TRA] ,mkoa wa Arusha pamoja na Halmashauri zinazounda mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wafanyabiashara wa Mkoa huo na kujiepusha na bughudha za ukusanyaji kwa wafanyabiashara.
Makonda amebainisha hayo kwenye Tuzo za Mlipakodi bora wa mwaka 2023/24 mkoa wa Arusha, Hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mount Meru Jijini Arusha, akiipongeza TRA pia kwa kuendelea kupunguza malalamiko ya kikodi kutoka kwa wafanyabiashara.
Katika sehemu ya Hotuba yake Makonda kando ya kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2023/24, amewataka wadau wa makusanyo ya serikali kuendelea kujenga mahusiano mazuri na walipakodi ili kuhakikisha Biashara zao zinakua badala ya kufa kwa kukamuliwa na TRA.
Wakati huo huo Chama cha waongiza utalii TATO,kimewataka wafanyabiashara wa sekta ya utalii wakiwemo wanachama wao kuhakikisha wanafuata sheria wanapoendesha shughuli za utalii ikiwa ni pamoja na kuwa walipakodi wazuri na hivyo kukiongezea sifa chama hicho.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji wa TATO,Elirehema Matolo katika hafla ya TRA ya utoaji Tuzo kwa mlipakodi ambapo taasisi hiyo iliibuka kinara na kupokea Tuzo ya mlipa kodi.
“Tatoo ni taasisi ya utalii inayoendesha shughuli za utalii na tumekuwa tukisisitiza sana kwa wanachama wetu kuhakikisha wanafuatilia masuala ya kodi kwa kufuata sheria za nchi ili kuwa walipaji wazuri wa kodi na kuhakikisha biashara ya utalii inachangia maendeleo na uchumi wa taifa ”
Alisema TATO imekuwa ikishirikiana vizuri na Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Arusha kwa kuwaalika ili kuzungumza na wanachama wao kuhusu changamoto za kikodi pindi zinapojitokeza ili kuhakikisha wanachama wao wanalipa kodi zinazostahili.
“Tato inapenda kila mwanachama wake awe mchangiaji mkubwa wa kodi na tumekuwa tukisisitiza kuwa hakuna mwanachana anayeweza kujiunga na Tato bila kuwa na Tax cl nanhiki ni kigezo ambacho tumekuwa tukikitumia katikankusajiri wanachama”
Hivyo tunazidi kuwahamasisha wananchi na wafanyabiashara mbalimbali kuhakikisha wanafuata sheria kwa kulipa kodi ipasavyo ili nchi yetu iweze kustawi kiuchumiii.