Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promosheni,Alex Msama akitia saini kitabu cha maombolezo na kushiriki dua ya kumuombea Alhaj Omary Mchengerwa, Baba mzazi wa Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mjini Makkah, Saudi Arabia, alipokuwa akitekeleza ibada ya Umrah.
Dua hiyo imefanyika leo, tarehe 24 Februari 2025, nyumbani kwa Mhe. Waziri Mchengerwa, Masaki, Jijini Dar es Salaam.