Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Banali amewashauri Wazazi na walezi kuwajengea mazingira bora ya matumizi ya vifaa vya mawasiliano watoto wakike wanaowanunulia simu ili kuwaepusha na unyanyasaji mitandaoni.
Kauli hiyo ameitoa katika shule ya wasichana Songe iliyoko katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wakati akitoa Elimu juu ya matumizi sahihi ya vifaa hivyo vya Mawasiliano pamoja na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii pindi wanapohitimu na kurejea shuleni wakati wa likizo.
” Wazazi tunawajibu wakuwasaidia watoto wetu katika matumizi sahihi ya hivi vifaa vya Mawasiliano kama Mtoto atapakia picha mtandaoni zisizo faa sasa badae ukija mzazi kuziona utajisikiaje kwahiyo tunaowajibu wakuwasaidia matumizi sahihi ya mitandaoni”Alisema Eng Imelda Banali Meneja TCRA kanda ya ziwa.
Wanafunzi katika shule ya sekondari ya wasichana songe wameipongeza mamlaka ya mawasiliano TCRA kuja na mpango huo kwani utasaidia kundi hilo kukabiliana na matumizi mabaya ya mitandaoni na ukiangalia wasichana ndio kundi ambao niwahanga na wathirika wakubwa wamitandao ya kijamii.