Jumuiya ya umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Geita imewataka Baadhi ya wabunge pamoja na Madiwani wanaopitisha katika Maeneo mbalimbali na kuhalalisha mitano tena kupitia nafasi zao kuacha mara moja kwani ni kosa kwa mujibu wa taratibu za Chama
Hayo ameyaeleza Mwenyekiti wa Umoja huo Manjale Magambo wakati alipofanya ziara ya kutembelewa wanachama wa jumuiya hiyo wilayani Nyangh”wale kwa lengo la kuhamasisha vijana kujitokeza kuchukua fomu za uongozi , kuona uhai wa chama hicho pamoja na kuchangamkia fursa za Mikopo ya asilimia 10.
“Tumekuja kuwaambia nafasi ya Rais tujiandae tumeshamaliza lakini tunabakiwa na nafasi ya ubunge na nafasi ya udiwani na hapa nataka tusikilizane vizuri tumemshuhudia mara kadhaa na kwa nyakati tofauti katibu mkuu wetu wa chama cha mapinduzi taifa Balozi Emmanuel Nchimbi akisisitiza kuna baadhi ya maeneo wabunge na madiwani wameanza kujipa mitano tena wanapita wanasema wanaanda maazimio ya mitano tena hiyo siyo taratibu ya chama chetu , ” Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo.
” Tunasema taratibu ya chama chetu kwa wakati huu tunawapa wabunge na madiwani nafasi ya kumalizia muda wao tunawaomba wale ambao wanatamani kupata hizi nafasi wakati wa chama cha mapinduzi bado na wabunge na wao wasijihalalishie mitano tena mbunge mmemsikia hapa akisema hii sio hati miliki wala sio hati miliki ya Mtu wakati ukifika kipenga kikipulizwa itakuwa ni uhuru kwa wote , Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo.
Hussen Kasu ni mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kugombea nafasi mbalimbali utakapokaribia uchaguzi mkuu ambapo amesema kila mtu atajipanga kueleza kile ambacho amekifanya kwa kipindi chote cha miaka yote mitano.
” Tunaemda kujenga Makalavati 12 kutokea karumwa mpaka hapa nyijundu na pia tunaemda kuiwekea molamu kazi hizo anazifanya Mama Samia na Jana nilimwambia mwenyekiti nafasi hii ya ubunge nafasi ya urais haina hati miliki wananchi wangu hawa walinijaribu mwaka 2010 wakasema hebu tumjaribu huyu nimefanya nao miaka 5 wakaniongeza 5 ikawa 10 nimefanya wakaniongezea tena 5 ninaeda kuimalizia bado miezi 4 niwe na miaka 15, ” Mbunge wa Nyangh”wale Hussen Kasu.