Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Nyang’hwale iliyopo wilayani humo Mkoani Geita wamekabidhiwa Runinga pamoja na Kisimbuzi kwa ajili ya kufatilia Maenddleo ya Miradi yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Makabidhiano hayo yamekuja Baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Geita , Manjale Magambo kufanya ziara wilayani Nyangh”wale ya kukagua uhai wa chama cha mapinduzi , kuhamasisha vijana kushiriki katika Uchaguzi mkuu sambamba na kuwataka vijana kuchangamkia fursa za Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.
” Tulifika hapa Ahsubuhi tukakutana na wanafunzi wenzetu kwa sababu ni moja pia ya maelekezo ya Dkt.Samia Suluhu Hassan na chama cha Mapinduzi kusikiliza na kutatua kero hasa za wanafunzi wanapokutana shuleni lakini moja ya Mambo ambayo tumekutana nayo walilizika kwanza na kazi Dkt.Samia Suluhu Hassan anayoifanya hasa kwenye uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu , ” Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo.
Na wakaomba kama Mwenyekiti wa Vijana wa Mkoa nitalidhia niwapatie TV ili wawe wanafatilia kazi zinazofanywa na serikali yetu zilizo chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ili pia na wao wawe mabalozi wema wa kazi za Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jambo hilo jema na mimi mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Mkoa kwa sababu tuna mapenzi mema Dkt.Samia Suluhu Hassan tukawaaidi kwamba tv inapatikana leo leo , ” Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa, Manjale Magambo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingalame akiwa katika Makabidiano hayo amempongeza Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo kwa ziara ambayo anaifanya ya kuzunguka kata kwa kata katika kila wilaya sambamba na kukagua na kuangalia uhai wa chama.
” Kwakweli kama Geita kuna kitu walifanya ni kuchagua wewe kuwa Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Geita ni kijana ambaye unafanya kazi nzuri na ninakufatilia nakuona ukitembelea kwenye wilaya mbalimbali mi nikuombee tuu kheri kwa Mwenyezi mungu na akujalie kila lililojema katika Majukumu yako kazi , ” Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, Grace Kingalame.
” Kwa kweli leo nina furaha kubwa mno Baada ya kupokea ziara ya Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM mkoa wa Geita , Komredi Manjale ametufikia hapa Nyang’hwale ahsubuhi tumezungumza naye tukamweleza changamoto tulizo nazo na kwasababu yeye ni msikivu na hii ni kazi kubwa ya chama cha mapinduzi tumepokea TV, ” Mkuu wa shule ya Sekondari Nyang’hwale, Zabron Seleman