Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA imetoa semina kwa mafundi wa kufunga mifumo ya umeme kwenye majengo Mkoani Kagera lengo ikiwa ni kuwakumbusha umuhimu wa majukumu yao ikiwa ni sambamba na kueleweshana mambo ya kuepukana nayo ili yasilete madhara katika kazi zao.
Semina hiyo imefanyika katika manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera ikiwashirikisha mafundi kutoka Wilaya zote za Mkoa Kagera,ambapo semina hiyo imeongozwa na Meneja wa EWURA kanda ya ziwa George Mhina akiwa na wataalamu mbalimbali kutoka kwenye mamlaka hiyo.
Mhina amewataka mafundi hao kuendelea kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao huku akiwataka wananchi kuwa makini na mafundi wanaowatumia kwa kuhakikisha wanakuwa na leseni ili kuepukana na changamoto kubwa pindi linapotokea tatizo kwenye mfumo wa umeme waliofungiwa.
Kwa upande wake Afisa mahusiano kwa wateja kutoka Tanesco Mkoa wa Kagera Lilian Mungai ameeleza kuwa kuwepo kwa mfumo mpya wa kuomba umeme unaoitwa Nikonekt umesaidia kwa asilimia kubwa kupunguza vishoka na matapeli kwa wateja wao maana kila kinafanyika kwenye mfumo