Siku mbili baada ya kuachana na kocha wake Tony Pulis, klabu ya Crystal Palace leo ilijitupa kwenye uwanja wa Emirates Kucheza na Arsenal katika mchezo wa kwanza wa EPL.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa mwisho wa siku ya leo kwenye EPL umeisha kwa matokeo ya ushindi wa 2-1 kwa Arsenal.
Palace walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Gunners kupitia Hangeland dakika 35, kabla ya Koscienly kusawazisha dakika 45.
Kipindi cha pili Arsenal walitengeneza nafasi nyingi lakini wakashindwa kuzitumia vizuri na mpaka dakika 90 bado ilikuwa 1-1, dakika 5 za nyongeza Aaron Ramsey akaifungia Gunners goli la ushindi.
Arsenal: Szczesny 6, Debuchy 5.5, Chambers 6.5, Koscielny 7, Gibbs 6 (Monreal 53), Arteta 5.5, Wilshere 7 (Oxlade-Chamberlain 69), Ramsey 6.5, Cazorla 5.5, Sanchez 6, Sanogo 5 (Giroud 62)
Substitutes not used: Rosicky, Martinez, Campbell, Coquelin
Scorers: Koscielny 45; Ramsey 90
Booked: Chambers, Cazorla
Crystal Palace: Speroni 6.5, Kelly 6.5, Hangeland 6, Dann 7 (Delaney 74), Ward 6.5, Puncheon 6, Jedinak 7, Ledley 7, Bolasie 6 (O’Keefe 90), Chamakh 7.5, Campbell 6.5 (Gayle 85)
Substitutes not used: McCarthy, Hennessey, Murray, Bannan
Scorer: Hangeland 35
Booked: Puncheon, Kelly, Chamakh
Sent off: Puncheon
Referee: Jonathan Moss
Attendance: 59,962