Baada ya mechi za mchana, ligi kuu ya England imeendelea usiku huu kwa mchezo mmoja kati ya Everton waliowakaribisha Arsenal.
Matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Goodison Park ni sare ya 2-2.
Everton walianza kufunga kupitia Coleman na Naismith katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Mpaka kufikia dakika ya 80 Everton bado walikuwa wakiongoza kwa 2-0, lakini kuingia kwa Santi Cazorla, Oliver Giroud na Campbell kulibadili mcheO na Gunners wakafanikiwa kurudisha magoli yote kupitia Ramsey na Giroud.
Ligi hiyo inaendelea tena kesho kwa mechi ya Man United vs Sunderland.