Kwanza shukrani zikufikie popote ulipo ewe mtu wa nguvu ambae siku zote umekua ukiisupport na kuwa karibu na Clouds Media.
Sasa taarifa ikufikie kwamba ofisi hii itampa Managing Director Joseph Kusaga na timu yake uwezo wa kufikia masoko yote ya ukanda wa Caribbean.
Clouds media International yenye makao yake makuu Abu Dhabi imefungua ofisi mpya huko Kingston Jamaica zitakazohudumia ukanda wa Caribbean na kufungua fursa za kibiashara kwa kampuni tanzu za Clouds Media.
Mkurugenzi mtendaji Joseph Kusaga amesema ufunguzi huu ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu kuiwezesha kampuni yake kujitanua kimataifa ikiwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji vipindi, utoaji wa huduma za ziada kupitia simu za mkononi, masoko na usimamizi wa matamasha bila kusahau matumizi ya solar na vyombo vya habari.
‘Jamaica na Caribia kwa ujumla ni soko jipya kwetu na kama Clouds mara zote huwa tunafikiria ni kwa namna gani tunaweza kujipenyeza katika masoko mapya ili kujitanua na kufanya biashara endelevu hivyo tunaona hii ni sehemu ya muafaka wa bidhaa na huduma tunazotoa’ – Joseph Kusaga
Ufunguzi huu wa ofisi unakuja ikiwa haujapita hata mwaka toka Clouds Media International ilipofungua ofisi zake Abu Dhabi ili kujitanua kimataifa na pia kuwezesha uwepo wa vyombo vyake vya habari kwenye ukanda wa Mashariki ya kati pamoja na uzinduzi wa kituo pekee cha Television huko mashariki ya kati chenye maudhui ya kiafrika kiitwacho Clouds TV International (CTVI) kinachopatikana kwenye ukanda maalum wa mamlaka ya vyombo vya habari Abu Dhabi.
Shughuli zote za Clouds International zitasimamiwa na Dean Mundy, mtayarishaji wa muziki wa rege na mfanyabiashara mzawa wa Jamaica mwenye uzoefu katika ukanda huo ambapo kukamilika kwa uzinduzi wa ofisi hizi kunadhihirisha umakini wa Clouds kujitanua kimataifa.
‘Ni zaidi ya muongo mmoja sasa toka nilipokutana na Joe na wenzake nilipokuja Dar es salaam kwenye tamasha la Fiesta na haikunichukua muda kutambua kuwa hii ni kampuni ambayo tunaweza kufanya nayo kitu, japo kwa hakika sikujua ni kivipi ila kwa sasa uhakika ninao na pia fursa zipo, tuko tayari kufanya vitu vikubwa hapa Jamaica’ – Mundy
Pamoja na Clouds Media International, makampuni tanzu kama status communications, Primetime International na Ray’s Solar yatakua na makao yake Kingston ambapo status communications itajihusisha na utoaji huduma za ziada kupitia simu za mkononi, Primetime Internationa itasimamia uandaaji wa matamasha na usimamizi wa Wasanii huku Ray’s Solar ikitoa huduma za umeme wa mionzi ya jua.
Mkurugenzi wa Status Communications Omari Salisbury amesema hivi karibuni alipotembelea Kingston ameona fursa ni nyingi sana huko Caribbean na kusisitiza ‘nilichokiona Jamaica kilinishangaza na kunionyesha kwamba ni sehemu nzuri ya kuwekeza na ni matarajio yangu kuiendeleza Status Communications na Clouds Media Jamaica