Rais wa awamu ya pili nchini Kenya Daniel Arap Moi ametimiza umri wa miaka 90 Septembe 2 2014 ambapo ameitumia siku hii kuzungumza na Wakenya na kupinga shinikizo la kutaka kufanyika kwa kura ya maoni ili katiba ibadilishwe kama unavyotaka muungano wa Cord na baadhi ya Magavana.
Muungano wa CORD tayari umekusanya saini milioni 1.4 kushinikiza kufanyika kura ya maoni ambapo muungano huu umelenga kukusanya saini milioni 5.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 52 nchini Kenya amewauwa watoto wake wawili kwa kuwatupa mtoni kisha na yeye akajinyonga muda mfupi baadae huku chanzo kikitajwa kutokana na mzozo wa kifamilia.
NYINGINE:
Siku kadhaa baada ya ripoti kuonyesha kwamba Polisi nchini Kenya huua kwa risasi raia wasio na hatia mara tano kuliko wanavyoua Majambazi, kundi la kutetea haki za binadamu la Muhuri limekwenda Mahakamani likitaka kufufuliwa kwa maiti ya msichana wa miaka 14 anaedaiwa kuuwawa na Polisi.
Ripoti hizi zikitoka Radio Jambo Kenya, zimesema msichana huyu anadaiwa kuuwawa na Polisi kwa risasi wakati wakiwasaka Watuhumiwa wa Ujambazi ambapo kundi hili linataka mwili huo ufanyiwe upasuaji kusaidia uchunguzi wa mauaji ya kiholela yanayofanywa na Polisi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB