Ni taarifa kutoka bungeni ambayo itasaidia kukata kiu ya waliokua wanaisubiria au wanasubiri kufahamu kuhusu katiba mpya ambayo imekua ikiundwa, kama itatumika kwenye uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Ripoti kutoka 104.4 Dodoma zinaamplfy kwamba katiba ya zamani ndio itakayotumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka kesho 2015 lakini itafanyiwa marekebisho ambayo ni 1. kumpa ruhusa mgombea binafsi kugombea, 2. kuwa na tume huru ya uchaguzi ya kusimamia uchaguzi, 3. mshindi wa Urais ashinde kwa zaidi ya asilimi 50, 4. matokeo ya uchaguzi wa Urais yaweze kupingwa Mahakamani, 5. kuwe na tume huru ya kusimamia uchaguzi.
‘Vyama vya siasa vinavyopenda kupendekeza mambo mengine ya kurekebisha katika katiba ya Jamuhuri ya muungano ya mwaka 1977 vinaombwa kufanya hivyo mapema’ – John Cheyo
Haya yametokana na kikao kilichofanyika kati ya Rais Kikwete na kituo cha demokrasia Tanzania ambapo Mwenyekiti wa kituo hicho John Cheyo.
Stori nyingine kuhusu hii ishu utaisikiliza kwenye Amplifaya ya CloudsFM kuanzia saa moja usiku leo ila usisahau kuniachia maoni yako hapa chini mtu wangu, unaonaje hiki walichoafikia?
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB
Unaweza kusikiliza ripoti nzima ya Simon Simalenga kutoka Bungeni kwa kubonyeza play hapa chini…