Mchaka mchaka wa ligi kuu ya England umeendelea tena jioni hii kwa mchezo uliowakutanisha vilabu viwili vilivyokuwa vikishika nafasi ya kwanza na ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya England – Chelsea dhidi ya Swansea.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la nyumbani la Chelsea Stamford Bridge umeisha kwa ushindi wa 4-2 kwa vijana wa Jose Mourinho.
Swansea walikuwa wa kwanza kupata goli baada ya John Terry kujifunga katika dakika za mwanzo za mchezo kabla ya Diego Costa kusawazisha mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Chelsea walirudi na kasi ya ajabu na kufanikiwa kupata mabao mawili haraka haraka kupitia Diego Costa tena ambaye leo alifunga hattrick.
Loic Remy akiingia kuchukua nafasi ya Diego Costa alifunga goli la nne kabla ya Jonjo Shelvey kuifungia Swansea goli la pili.
Mpaka refa wa mchezo Mark Claternburg anapuliza filimbi ya mwisho matokeo yalikuwa 4-2.