Hatimaye ligi ya mabingwa wa ulaya imeanza tena kwa michezo kadhaa kupigwa usiku wa leo huku mabingwa wa watetezi Real Madrid wakianza kuutetea ubingwa wao kwenye mchezo dhidi ya FC Basle.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu umeisha kwa matokeo ya ushindi mzito kwa Real Madrid walioibamiza Basle 5-1.
Suchy alianza kujifunga goli kwenye dakika ya 14 na kuipa uongozi Madrid, kabla ya Gareth Bale kufungua ukurasa wake wa magoli kwenye UCL kwa kufunga goli la dakika ya 30, Cristiano Ronaldo akaongeza lingine dakika ya 31, James Rodriguez akafunga goli la 4 dakika ya 36, na Karim Benzema akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la FC Basle dakika ya 79.
Timu zilipangwa hivi:
Real Madrid: Casillas, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo, Nacho, Kroos, Rodriguez, Bale, Modric, Ronaldo, Benzema.
Subs: Navas, Varane, Fabio Coentrao, Hernandez, Arbeloa, Isco, Illarramendi.
Goals: Suchy OG 14, Bale 30, Ronaldo 31, Rodriguez 36, Benzema 79
Basle: Vaclik, Samuel, Schar, Suchy, Safari, Zuffi, Frei, El-Nenny, Xhaka, Streller, Gonzalez.
Subs: Vailati, Delgado, Gashi, Kakitani, Aliji, Embolo, Calla.
Goal: Gonzalez 37
Referee: Damir Skomina (Slovenia)