Katika mchezo mwingine wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa ulaya, klabu ya Arsenal leo ilikaribishwa na Borrusia Dortmund katika mchezo wa kwanza wa kundi D.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa BVB – Signal Iduna Park, umeisha huku Arsena wakipokea kipigo cha kwanza kwenye michuano baada ya kufungwa 2-0.
Cirro Immobile alianza kuifungia Dortmund katika kipindi cha kwanA kabla ya Pierre-Emerick Aubameyang kufunga goli la pili dakika ya 48.
Danny Welbeck itabidi ajilaumu mwenyewe kutokana na kupoteza nafasi 3 za wazi za kufunga kwenye mchezo.
Arsenal mechi ijayo watacheza na Galatasary ambao leo hii nao waliotoka sare dhidi ya Anderletch.