Siku chache baada ya kushindwa kupata matokeo chanya katika mchezo wao wa pili wa ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya klabu ya AS Roma, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City leo walisafiri mpaka Villa Park kwenda kuchuana na Aston Villa.
Mchezo huo uliokuwa wa kasi umemalizika hivi karibuni huku City wakifanikiwa kuwasogolea Chelsea kwenye msimamo wa ligi kuu ya Barclays.
Huku zikiwa zimebakia dakika 10 mchezo kumalizika Yaya Toure aliiandikia City goli la kwanza kabla ya Sergio Aguero kuihakikishia ushindi timu ya Manuel Pellegrini kwa goli zuri kabisa alilofunga katika dakika ya 88.
Aston Villa inayofundishwa na Paul Lambert akisaidiwa na nahodha wa zamani wa Man United, Roy Keane, walijitahidi kwa kila hali kujaribu kupata matokeo mazuri dhidi ya mabingwa watetezi lakini bahati haikuwa yao, na mpaka mwamuzi anamaliza mpira City walikuwa wamewafunga nyumbani kwao kwa magoli 2-0.
Timu zilizpangwa kama ifuatavyo:
Aston Villa: Guzan, Hutton, Senderos, Baker, Cissokho, Cleverley, Westwood, Delph, Richardson (Grealish 71), Weimann (Benteke 61), N’Zogbia (Bacuna 71)
Subs (not used): Clark, Bent, Sanchez, Given
Bookings: NONE
Goals: NONE
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov, Milner, Fernandinho (Lampard 56), Toure, Silva (Navas 84), Dzeko (Fernando 64), Aguero
Subs (not used): Sagna, Caballero, Jesus Demichelis, Jovetic
Bookings: Kolarov
Goals: Toure (82), Aguero (88)
Referee: Chris Foy (Merseyside)
Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2780485/Aston-Villa-0-2-Manchester-City-Yaya-Toure-Sergio-Aguero-earn-Manuel-Pellegrini-late-win.html#ixzz3FCgc0CEd
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook