UHURU
Hali ya uchafu nje ya machinjio ya vingunguti Dar es salaam imezidi kuwa mbaya na kuhatarisha afya za walaji hususan wateja wanaonunua nyama nje ya machanjio hiyo.
Kwa muda mrefu kumekua na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa machinjio huku wakiuza nyama hizo katika maeneo machafu na nyama nyingine zikitajwa kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Imebainika kuwa nyama hizo huuzwa kwa mafungu kwa bei ya kutupa zikiwemo ambazo hazijapimwa na kuwekwa alama maalum na wataalam wa afya.
Baadhi ya wananachi wamewalalamikia watendaji wa Manispaa ambao hufika na kukusanya ushuru bila kuangalia hali ya usafi katika eneo hilo.
UHURU
Watendaji wa Serikali pamoja na wanasiasa wametajwa kuwa vinara wa uhujumu uchumi kwa kukiuka sheria kwa makusudi kwa maslahi binafsi.
Habari za kuaminika zinasema baadhi ya watendaji na watumishi wa Serikali wamekua wakitumia kampuni za watu binafsi kupewa zabuni mbalimbali kwenye Halmashauri nchini.
Tayari taarifa za ukaguzi wa Halmashauri hizo zimefikishwa kwenye Taasisi ya kuzuia rushwa kwa hatua zaidi kutokana na kubainika kwa viashiria vya rushwa.
MTANZANIA
Baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na msanii wa filamu Aunty Ezekiel kuvinjari nchini Marekani hatimaye waziri huyo amefunguka.
Nyalandu alisema tuhuma hizo zimetengenezwa na kundi la watu ambalo miongoni mwao ni baadhi ya viongozi wa Serikali ambao humchafua kutokana na utendaji kazi wake.
Nyalandu alisema alikwenda Marekani septemba12 kwa ajili ya kufungua tamasha la utamaduni na utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ambako alikutana na msanii huyo mara moja pamoja na mwingine wa Bongo Fleva Kassim Mganga usiku katika moja ya maeneo nchini humo.
Alikana kutanua na msanii huyo kama baadhi ya nyombo vya habari vilivyoripoti na kusema maneno hayo ni kwa lengo la kumwaribia heshima yake mbele ya jamii.
MTANZANIA
Ugonjwa wa Rubella uliodhaniwa kuwa ni Surua umezidi kusambaa kwa wingi Mkoani Mtwara na hadi sasa umefikia idadi ya wagonjwa 570 wanaoumwa Wilayani Newala.
Mratibu wa magonjwa ya kuambukiza Shira Mangabe alisema ugonjwa huo pia umeingia Wilaya ya Masasi mjini ambapo wagonjwa10 wamegundulika kuumwa.
Alisema ugonjwa huo umekua ukiwatesa zaidi watoto wa shule za Msingi na ulianza katika shule ya Mkoma na kusababisha shule hiyo kufungwa kwa muda kutokana na wanafunzi kuambukizana.
NIPASHE
Mahakama kuu Tanzania kanda ya Dar es salaam imefuta mwenendo wa kesi ya mauaji iliyofunguliwa katika mahakama ya Kisutu dhidi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Gabriel Fuime na wenzake 11 wanaohusika na kuporomoka kwa jengo la gorofa 16 katika mtaa wa Indira Gandh na kuua watu 27 badala yake imeamuru wafunguliwe mashtaka ya kuua bila kukusudia.
Amri ilitolewa na Jaji Salvatory Bongole baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa mbele yake na mawakili upande wa utetezi.
Alisema watuhumiwa kuendelea kushtakiwa kwa makosa ya zamani ya kuua bila kukusudia badala ya makosa ya mauaji hivyo wanastahili kuwa nje ya dhamana zao.
MWANANCHI
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kigezi iliyopo Chanika Dar ameozeshwa kwa mkazi wa kijiji cha Mbonde Halfa Ally mwenye miaka54 ambaye humfungia ndani ili wakazi wa eneo hilo wasimuone.
Mama wa mtoto huyo alisema jana kuwa alipata taarifa za mwanaye kuozeshwa kutoka kwa mdogo wake ambaye alikua akiishi karibu na nyumba ya baba wa mtoto huyo.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo za mtoto huyo ambaye alikua akiishi na baba yake mzazi alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa na baadaye kukamatwa kwa mzazi mwenzie lakini alishangaa baadaye kuachiwa huru bila kuchukuliwa hatua zozote.
HABARILEO
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Hawa Ghasia amekataa kupiga picha ya pamoja na walimu wa Sekondari ya Mafiga Manispaa ya Morogoro kwa madai kuwa na matokeo mabovu ya wanafunzi licha ya kuwepo walimu wa kutosha.
Alisema amechukua uamuzi huo baada ya kubaini wapo walimu68 lakini wameshindwa kufaulisha wanafunzi na kufanya shule kuambulia daraja la sifuri kwa kiwango kikubwa.
Waziri huyo ambaye alikua katika ziara ya siku moja Mkoani Morogoro alikwenda shuleni hapo kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo alishangazwa pia na idadi ndogo ya vyumba vya madarasa huku wanafunzi wakipokeza kuingia darasani lakini kuwepo na idadi kubwa ya walimu ambao hukaa muda mwingi bila kuwa na kazi za kufanya.
HABARILEO
Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru amewataka vijana wa CCM kuisoma na kuielewa katiba mpya inayopendekezwa kwani ni bora kuliko katiba nyingi za Afrika.
Alisema sasa ni wakati wa vijana kuisoma katiba na kuielewa na si kukubali kupotoshwa na Ukawa kwani imezingatia makundi yote ndani ya jamii ya Watanzania .
Alisema mbali ya Ukawa kutaka kupotosha wananchi kwa lengo la kuipinga Katiba lakini anashukuru imeeleweka na itafanyiwa kazi ili Watanzania waweze kunufaika nayo kwa siku za baadaye.
HABARILEO
Shehena ya Salfa ilioyachwa Wilayani kisarawe na Mamlaka ya Reli Tanzania TAZARA baada ya treni yake ya mizigo kupata ajali huenda ikiwa tatizo kubwa kwa Taifa endapo itachelewa kutolewa.
Baadhi ya wananchi walisema kuungua kwa shehena hiyo kumewatia hofu kubwa kutokana na kutambua kuwa kemikali hizo zina madhara kwa binadamu hasa zinapoingia kwenye maji na kusambaa kwenye hewa.
Aidha katika kipindi hiki ambacho mvua zimeendelea kunyesha wananchi wanahofu kwamba maji yanaweza kwenda kuingia kwenye mto Mpiji ambapo maji yake yanakutana na mto Msimbazi ambayo yanatumiwa na wakazi wengi wa Dar es salaam na huenda yakahatarisha maisha ya watumiaji.
NIPASHE
Miss Tanzania Sitti Mtemvu kutoka kanda ya Temeke amesema licha ya baba yake kupanda jukwaani kumpongeza alimkataza kushiriki kinyang’anyiro hicho cha kuwania taji hilo lililofanyika ukumbi wa Mlimani City mwishoni mwa wiki.
Sitti ambae baba yake mzazi ni Mbunge wa Temeke Abass Mtemvu alizawadiwa kiasi cha Milioni10 lakini amekiri baba yake hakuwa tayari mwanae kushiriki mashindano hayo.
Alisema baba yake alimkubalia dakika za mwisho kwa shindo upande ambapo safari ya Miss Tanzania ilianzia kitongoji cha Chang’ombe hadi kushinda nafasi hiyo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Fs