Mume na mke wamejilipua namafuta ya Petrol Mkoani Mtwara baada ya kutokea kwa ugomvi baina yao wakati wa usiku.
Kamanda wa Polisi alisema vifo hivyo vilitokana na ugomvi wa kifamilia ambapo Mume huyo aliyetambulika kwa jina la Selsius Kamguna alimpiga mkewe hadi kupoteza fahamu.
Alisema baada ya kuona mke wake amepoteza fahamu aliamua kuteketeza nyumba yao kwa moto akitumia mafuta ya petroli wakiwa ndani kitendo kilichosababisha wote wawili kupoteza maisha,
MWANANCHI
Mgogoro wa kifamilia kuhusu mwenye haki ya kuzika mwili wa Rosemary Marandu umeingia siku ya43 leo huku ukiendelea kuhifadhiwa katika hospitali ya KCMC Moshi.
Mwili wa marehemu huyo aliyefariki dunia Septemba4 umehifadhiwa hospitalini hapo na unalipiwa shilingi 9,000 kwa siku na gharama mpaka sasa kufikia 387,000 huku baba wa marehemu akitoa ruksa ya kuuzika huku akisema hana mamlaka ya kuzuia kuzika mke wa mtu.
Mume wa marehemu Sigfrid Mling alisema baba mkwe wake ndiye anaekwamisha mazishi ya mkewe huku akitoa lugha chafu.
Alisema mbali na baba mkwe wake pia ndugu wa karibu wa marehemu wamekua hawatoi ushirikiano katika kupanga mazishi ya ndugu yao huyo hali inayochangia zoezi hilo kuwa gumu zaidi.
MWANANCHI
Mkoa wa Dodoma bado unakabiliwa na utoro wa wanafunzi jambo linalosababisha idadi kubwa ya vijana kuzurura mitaani.
Ofisa elimu Mkoa wa Dodoma Juma Kaponda amesema kumekua na mwitikio mdogo wa wanafunzi katika shule mbalimbali za Sekondari na msingi kutoka na wengi kujihusisha na biashara kwa ajili ya kujipatia kipato huku wanafunzi wa kike wakiacha shule kutokana na ujauzito.
Akitolea mfano sekondari ya Chikopelo mwaka 2011 ilipokea wanafunzi 103 wa kidato cha kwanza lakini wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu wakiwa ni saba kutokana na wengi kuacha shule.
MWANANCHI
Kashfa imendelea kumwandama Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas baada ya vielelezo mbalimbali kuonyesha kuwa ameghushi umri wake.
Sitti katika fomu zake alijaza ana miaka18 kitendo ambacho kimeshtua wengi na kuanza kufuatilia taarifa zake na kubaini ana miaka25.
Kwa mujibu wa kanuni za ushiriki wa mashindano ya urembo, mrembo huyo ambaye alitokea Wilaya ya Temeke hakuna na sifa za kushiriki hivyo kutakiwa kuvuliwa taji hilo kwani tayari alishavuka umri uliowekwa kinanuni na waandaaji.
NIPASHE
Mtoto mwenye umri wa siku nne ameibwa baada ya mama yake kunyweshwa juisi inayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya Mkoani Dodoma.
Mganga hospitali ya rufaa Dodoma Nassor Mzee alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwanamke huyo Teddy Bishazila mwenye miaka18 alilazwa hospitalini hapo baada ya afya yake kuathiriwa na dawa hizo.
Akizungumzia kwa taabu tukio hilo mwanamke huyo alisema alijifungua mtoto huyo salama na kurejea nyumbani siku inayofuata ambapo dada mmoja aliyemsaidia mizigo siku anatoka kujifungua na alifika nyumbani kwake akiwa na juisi ambapo alimshawishi kunywa ili aongeze damu mwilini baada ya kujifungua.
Baada ya kunywa alijikuta yupo hospitali baada ya kupoteza fahamu huku akiwa hafahamu mtoto wake yupo wapi na alipouliza aliambiwa alichukuliwa na dada aliyekua amemsindikiza.
NIPASHE
Watu12 ambao ni madereva wa bodaboda Bukoba wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kufanya vurugu na kuvunja nyumba za watu kwa mawe huku polisi wakilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Chanzo cha vurugu hizo ni askari waliokua doria kumkamata mwendesha bodaboda mwenzao aliyevunja sheria na kusababisha wenzao kuandamana wakishinikiza atolewe.
Kaimu Kamanda wa Polisi Gilles Mroto alisema waliamua kumkamata mmoja wao kutokana na kukiuka sheria za barabarani ndipo walipomkamata kwa lengo la kumshtaki huku wenzao wakianza kufanya vurugu wakidai anaonewa.
Alisema tayari wamewakamata vijana 12 waliohusika na vurugu hizo na watawekwa ndani wakati uchunguzi wa mali zilizoharibiwa ukifanyiwa kazi.
HABARILEO
Watu wawili mama na mwanaye wameuawa kinyama na watu wasiojulikana wakisadikiwa kujihusisha na imani za kishirikina Mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea Oktoba14 saa 2 usiku wakati familia hiyo ikijiandaa kula chakula cha usiku ndipo kundi la watu lilipovamia nyumba hiyo na kufanya mauaji hayo ya kikatili.
Alisema mara baada ya kuingia walianza kuwavamia kwa kuwakatakata na mapanga sehemu mbalimbali za miili yao kisha kuwachinja shingo hadi kufariki dunia.
HABARILEO
Jamii za wafugaji nchini zinadaiwa kukabiliwa na kiwango kikubwa cha tatizo la kinamama kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa,mgongo wazi unaochangiwa na wajawazito kukosa vitamini inayotokana na mboga za majani kutokana na kitoweo chao kikubwa kuwa nyama.
Mwenyekiti wa Chama cha wazazi wa watoto wenye matatizo hayo Abdulhakim Bayakub alisema watoto 2000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo hilo na wengi wamekua wakicheleweshwa kufikishwa hospitalini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuamini imani za kishirikina.
Aliwataka wafugaji kupenda kuhudhuria kliniki na semina mbalimbali zitolewazo ili kuepukana na matatizo kama hayo ambayo yanaweza kuzuilika.
MWANANCHI
Mtoto wa kike wa miaka13 aliyenajisiwa na mwajiri wake ameeleza kuwa alimtaarifu mke wa mtuhumiwa kuhusu vitendo hivyo,lakini wenyewe wakasameheana na kumtaka asiwaambie watu.
Inadaiwa kuwa mtoto huyo ambaye alikua akifanya kazi za ndani maeneo ya Bunju B, Dar ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala alibakwa zaidi ya mara tatu na mwanaume huyo mwenye umri wa miaka35 ambaye alikua akimfanyia vitendo hivyo kwa nyakati tofauti.
Mtoto huyo akizungumza kwa taabu hospitali hapo alisema mara ya pili wakati akifanyiwa kitendo hicho mke wa mtuhumiwa aliwakuta na alipomuuliza mumewe anafanya nini akasema anamtania na ndipo walipoingia chumbani na baadaye mwanamke huyo kutoka na kumwambia mumewe ameomba msamaha hivyo asiseme kwa watu.
Mtoto huyo alisema yupo tayari kurudi kijijini kwao Bukoba kuendelea na shule lakini atafanya hivyo baada ya kulipwa fedha zake shilingi 160,000 za malimbikizo ya mshahara wake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook