Siku chache baada ya vyombo mbali mbali vya habari kuripoti kuhusiana na serikali ya Nigeria na kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram kufanya makubaliano ambayo yalijenga matumaini ya kuachiwa huru kwa wasichana zaidi ya 200 wanaoshikiliwa na kikundi hicho, shirika la utangazaji la uingereza BBC, limeripoti kuhusiana na mashambulizi yaliyofanywa na kikundi hicho.
Taarifa zinasema kwamba wapiganaji hao wamewaua kwa kuwapiga risasi na kuwachinja watu kadhaa katika vijiji vitatu tofauti Kaskazini Mashariki ya Nigeria, na kupandisha bendera yao.
Serikali ya Nigeria imesisitiza kuendelea na nia yake ya kufanya majadiliano na kikundi hicho, licha ya kuwa kimekiuka makubaliani waliyoafikiani mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Chad.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook