Baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili, usiku wa leo jumatatu Manchester United wakasafiri kwenda kuumana na West Bromwich Albion katika mchezo wa raundi ya 8 wa Barclays Premier League.
Mchezo uliopigwa katika dimba la Hawthorns umemalizika kwa klabu ya Manchester United kushindwa kupata matokeo chanya ugenini katika kipindi cha miezi zaidi ya 6, baada ya kutoka na sare ya 2-2.
WBA ndio walianza kufunga katika dakika ya 8 kwa goli zuri la Sessegnon, goli hili likadumu mpaka mapumziko. Kipindi cha pili United walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia Maroune Fellaini. Dakika kadhaa baadae Saido Beralinho akipafia WBA goli la pili, huku muda ukizidi kuyoyoma Daley Blind akaisawazishia Man United na kuipa sare ya 2-2.
TIMU ZILIPANGWA HIVI
West Brom 4-2-3-1: Myhill 7; Wisdom 7, Dawson 7, Lescott 7, Pocognoli 6; Gardner 7, Morrison 6; Dorrans 7.5, Sessegnon 7, Brunt 6.5; Berahino 7.
Subs not used: Daniels, Blanco, McAuley, Mulumbu, Gamboa, Anichebe, Ideye.
Goals: Sessegnon 8, Berahino 66
Booked: Morrison
Manchester United 4-3-1-2: De Gea 6; Rafael 6, Jones 6, Rojo 5, Shaw 5; Herrera 5.5 (Fellaini HT, 7), Blind 6, Di Maria 7; Mata 6; Van Persie 6, Januzaj 5.5.
Subs not used: Lindegaard, Smalling, Fletcher, Carrick, Fellaini, Young, Falcao.
Goals: Fellaini 48, Blind 87
Booked: Blind
MOM: Graeme Dorrans
Referee: Mike Dean