Siyo tetesi tena,sasa ni rasmi kwamba Waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye amekua akitajwa kuwania urais amethibitisha wazi kuwa atagombea urais katika uchaguzi mkuu mwakani.
Alitoa uamuzi huo juzi jijini Londoni ambapo yupo katika shughuli za kikazi hatua hiyo inaondoa uvumi ambao umekuwepo kwa takribani miezi mitatu na tayari ameingia katika kiny’ang’anyiro hicho.
Pinda aliweka nia ya kuelea Ikulu akisistiza kuwa hajatangaza rasmi lakini akasema kuwa anaanza harakati kimyakimya baada ya kuulizwa swali kuwa anafikiria ni kiongozi gani anafaa kurithi mikoba ya Jakaya Kikwete.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa kamati za bunge Zitto Kabwe amesema iwapo Serikali itashindwa kulipa deni la bilioni22.5 inayodaiwa na kampuni ya ABSA group ya nchini Afrika Kusini hadi kufikia Machi mwakani itapoteza asilimia 30 ya hisa zake katika benki ya biashara ya NBC.
Alisema endapo Serikali itashindwa kulipa deni hilo,benki hiyo itakua chini ya kampuni hiyo ambayo ina hisa asilimia55 wakati awali ilikua na hisa70 za benki hiyo lakini ikauza asilimia15 ya hisa zake kwa shirikia la fedha la kimataifa.
Ili kuinusuru Serikali Zitto amemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia mikataba yote ya Serikali na Absa katika benki hiyo ili kubaini kilichojificha.
Serikali ilikopa kiasi hicho cha fedha ili kutekeleza agizo la benki kuu ya Tanzania ambayo mwaka 2012 iliagiza NBC kuongeza mtaji wa biashara wenye thamani ya shilingi bilioni75 baada ya ule wa awali kushuka kwa asilimia 12.
MWANANCHI
Wauguzi wa Zahanati ya Kurugee Wilayani Butiama wanalazimika kutumia chemli wodini wakati wa kuwahudumia wagonjwa kutokana na kukosekana kwa umeme.
Mganga wa zahati hiyo Micoruah Simon alimwambia Meneja wa Shirika la umeme Wilayani humo kuwa awali walikua wakitumia karabai ambazo kwa sasa zimeishiwa gesi na halmashauri ya Wilaya hiyo haina fedha za kununulia gesi nyingine mpaka sasa.
Mbali na hilo Saimon alisema Zahanati hiyo inaupungufu mkubwa wa vifaa vya tiba na dawa zikiwemo za chanjo mbalimbali za watoto wachanga.
NIPASHE
Sakata lililojitokeza la mrembo wa Tanzania Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri limeingia katika sura mpya baada ya Baraza la sanaa la Taifa BASATA kueleza kuwa litamvua taji hilo endapo itabainika kweli alichakachua umri wake.
Katibu mkuu wa Basata Geogrey Mwingereza alisema Baraza hilo linasubiri uchunguzi ukamilike na endapo watabainika hawatakua na la kufanya zaidi ya kumvua taji.
Wakati Baraza hili likisema hivyo uongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo wanatarajia kukutana leo kwa ajili ya kujadili suala hilo baada ya kuwepo na mkanganyiko huo.
HABARILEO
Mtuhumiwa wa matukio ya kigaidi na umwagiaji watu tindikali katika miji mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Arusha Yahya Hassan maarufu kama Sensei amezikwa usiku wa manane kijijini kwao Dodoma.
Sensei aliuawa na polisi wakati akijaribu kuwatoroka baada ya kupambana nao wakiwa kwenye gari wakati akiwapeleka alipoficha silaha zake.
Shemeji wa marehemu ambaye hakutajwa jina lake alisema mwili wa marehemu ulizikwa juzi saa sita usiku kwa kile kinachoelezwa wanandugu walihofia kusumbuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Baba mzazi wa Sensei aliamuru mwili wa mwanae usafirishwe hadi nyumbani kwao na kuzikwa usiku huo baada ya kubainika mwili kuharibika kwa kiasi kikubwa na kuanza kutoa harufu kali.
MTANZANIA
Familia ya marehemu Salome Richard aliyedaiwa kufariki dunia kwa ugonjwa wa Ebola Wilayani Sengerema imeibuka na kusema mara baada ya kifo cha ndugu yao viongozi wa Serikali walichoma nguo zao zote.
Alisema kitendo cha kuchomwa nguo zao zote kimechangia zaidi wao kutengwa na jamii inayowazunguka huku wakiitwa ‘familia ya Ebola’.
Mume wa marehemu alisema wamekua wakiishi maisha ya taabu baada ya kufungiwa kwenye chumba kimoja huku wakipewa nguo nyeupe kwa ajili ya kuvaa na mpaka sasa madaktari hawajachukua vipimo vyovyote wala dawa na wamekua wakipewa magodoro huku wakitengewa sehemu ya kujisaidia wenyewe.
Anasema anasikitishwa na hali hiyo ya kuendelea kufungiwa wakati Serikali imetangaza hakuna Ebola nchini huku baadhi ya ndugu zake akiwemo mama yake mzazi kulalamika kuvimba miguu kwa kukaa sehemu moja muda mrefu.
MTANZANIA
Watu wawili wamefarki dunia Wilayani Muleba baada ya kula ugali wa muhogo unaosadikiwa kuwa na sumu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Henry Mwaibabe alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo mama na mtoto wake walifariki dunia huku ndugu wengine wanne wakiendelea kutibiwa hospitali.
Alisema familia hiyo ilinunua udaga kwa ajili ya kusaga unga na baada ya kuutumia hali zao zilibadilika na kukimbizwa hospitalini ambapo mama na mwanaye wa miaka mitano walifariki njiani kabla ya kufikishwa hospitali.
TANZANIADAIMA
MWENYEKITI wa Baraza la wanawake CHADEMA Halima Mdee amesema kuwa katika kipindi cha miaka tisa ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete deni la Taifa limeongezeka kutoka trilioni7 hadi30 huku kila Mtanzania bila kujali umri wake akitakiwa kulipa kiasi cha shilingi 680,000 kwa fedha ambazo hakushirikishwa wakati wa kuzikopa.
Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe alisema deni hilo limeongezeka kwa sababu ya kupeleka maendeleo kwa wananchi jambo ambalo alisema si kweli kwani katika kipindi hicho hali ya maisha ya wananchi imezidi kuwa duni.
Alisema Warioba aliamua kuweka suala la uadilifu na uwajibikaji katika rasimu ya pili ya katiba ili kuzuia viongozi wa umma wasiendelee kukopa fedha nje ya nchi badala yake wazilete kwa wananchi.
MTANZANIA
Kamati ya kudumu ya bunge la Serikali za Mitaa imepokea taarifa ya matumizi mabaya ya shilingi bilioni256 ya miradi ya maendeleo katika baadhi ya Halmashauri nchini.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Rajab Mbarouk alisema hayo jana wakati akipokea taarifa hiyo toka kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ya mwaka 2012/13.
Alisema fedha zilizotumika vibaya ni zile zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika halmashauri hizo ambapo alisema zipo fedha ambazo hesabu zake hazijapatiwa majibu na Halmashauri husika.
Alisema sababu za kupotea kwa fedha hizo imechangiwa na kutokuwepo na usimamizi mzuri wa sheria ya ununuzi wa umma pamoja na kuwepo mishahara hewa na fedha maalum ambazo ni asilimia tano kwa ajili ya mfuko wa akina mama na vijana.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook