Hali ni mbaya katika hospitali ya Ocean Road Dar es salaam kutokana na uhaba mkubwa wa dawa.
Wagonjwa wengi waliolazwa katika hospitali hiyo kwa nyakati tofauti wamesema wameshuhudia wenzao kadhaa wakipoteza maisha kwa kuwa taasisi hiyo haina dawa za kuwatibu.
Muuguzi ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuna mgonjwa alifariki jana kwa kukosa dawa huku ndugu zake wakipewa taarifa za kwenda kutafuta dawa lakini hawakurejea hadi ndugu yao alipopoteza maisha.
Katika baadhi ya maduka bei ya baadhi ya dawa walizoandikiwa wagonjwa bei yake ni kubwa hivyo kushindwa kumudu gharama zake.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete amesema kazi ya urais ni ngumu na anatamani amalize kipindi chake ili awe mtu huru kufanya mambo yake ikiwemo kilimo huku akiamini atapatikana rais bora kuingoza vizuri Tanzania kuliko yeye.
Rais aliyasema hayo akiwa Beijing China alipokua akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha mataifa yao.
“Ni kweli naona kama muda haufiki ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga ng’ombe na mbuzi wangu,nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha,”alisema JK
Alisema kazi ya urais ni ngumu sana na anawaonea gere wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye kazi hiyo kwa miaka mingi.
NIPASHE
Mbunge wa Kasulu Mjini Moses Machalli amesema kwamba bunge linakabiliwa na ukata wa fedha na kwamba hali hiyo inatishia wabunge kupoteza uadilifu kwani wanaweza kushawishika kuomba rushwa ili kujinusuru na hali ngumu ya maisha.
Alisema hali hiyo pia inawafanya wakose fedha za kununua mafuta ya kuweka kwenye magari wanayotumia na hivyo kujikuta wakisafiri kwa shida kwenda kuhudhuria vikao vya kamati.
Alisema licha ya bunge kuidhinisha mamilioni ya shilingi kutumika inashangaza kuona kamati za bunge zikikosa fedha za kuziwezesha kufanya ziara kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.
MTANZANIA
Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia benki ya stanbic tawi la Mayfair jijini Dar es salaam na kupora fedha zinazodaiwa kuwa zaidi ya shilingi milioni200.
Kamanda wa polisi kanda ya Kinondoni Camilius Wambura amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema hadi sasa watu13 wanashikiliwa na polisi wakiwawemo wafanyakazi tisa wa benki hiyo.
Alisema baada ya kuchukua fedha hizo watu hao waliondoka bila kujeruhi watu na kutokomea kusikojulikana na kwa sasa uchunguzi unaendelea ili kuja na majibu sahihi kubaini wizi huo.
MTANZANIA
Mji wa Moshi jana ulikumbwa na taharuki baada ya kuwepo na taarifa za mgonjwa anayehisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola akitokea nchin Senegal ambapo alilazwa katika Zahanati moja Mkoani humo.
Mganga mkuu wa Halmashaur ya Wilaya ya MoshiTimothi Wanang alikiri kuwepo mgonjwa huyo na kusema alifika katika Zahanati ya Iwa lakini kutokana na hali yake kubadilika alihamishiwa Zahanati nyingine iliyositisha kutoa huduma za afya kwa muda kwa wagonjwa wengine kutokana na hofu.
Alisema mgonjwa huyo ambaye alikua na dalili zote za ugonjwa huo alianza kutibiwa na madaktari ambao walivalia mavazi maaalum kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo huku watu wengine pamoja na wagonjwa kuondoka kwa hofu ya kuambukizwa.
HABARILEO
Mwanaume mmoja mwenye miaka30 amejinyonga kwa kamba ya katani baada ya kumuua mkewe kwa kumchinja shingo kwa kisu kutokana na kile alichodaiwa kudharauliwa na mkewe.
Tukio hlo lilithibitishwa na kamanda wa polisi Mkoa wa Singida Goefrey Kamwela ambaye alisema mwanaume huyo baada ya kuhakikisha mkewe amefariki alichukua kamba ya katani na kujitundika kwenye moja ya kenchi ya nyumba yake hadi kufariki.
Alisema kabla ya kufariki marehemu aliacha ujumbe kuwa amechukua uamuzi huyo baada ya mkewe kushirikiana na kaka yake kumuoza binti yake wa kufikia bila ridhaa yake.
HABARILEO
Walimu175 wa masomo ya Sayansi Mkoani Simiyu wameingia kwenye mgomo wa kutoshiriki semina iliyokua ikiendelea kwa kutofahamu kiasi cha posho watakacholipwa.
Walimu hao ni kati ya 200 kutoka Wilaya tano waliokua wakishiriki semina hiyo ambapo alisema barua za mwaliko ziliwaeleza kuwa semina itaka ya siku10 lakini walishangazwa siku kupunguzwa na kuwa tano.
Walimu hao walibainisha kuwa wamekua wakiishi maisha ya shida bila kupata posho za kujikimu tangu walipofika na kwamba walikua wanadaiwa fedha na wahudumu wa nyumba za kulala bila kujua watapata wapi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook