Watu 9 waliowasili jana Kenya wakitokea Liberia wamefanyiwa vipimo vya Ebola na kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo zimesema hakuna aliyeonekana kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
Katibu wa Afya wa Baraza la Mawaziri nchini Kenya, James Macharia amesema baada ya watu hao kuwasili nchini humo majira ya usiku, walipelekwa karantini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo hivyo ambapo hakuna aliyebainika kuwa na dalili za kuwa na Ebola.
Baadhi ya watu hao walikuwa wakifanya kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) Liberia.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook