Wakenya tisa kati ya kumi na mbili waliokua wamekwama nchini Liberia tangu kulipuka kwa ugonjwa wa Ebola wamewasili usiku katika uwanja wa Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) Nairobi, Kenya.
“..Awali tulikua tunatarajia wakenya 150 kutoka Liberia lakini ni kumi na mbili pekee walioonesha dharura ya kusafiri kurudi nyumbani, na kama mnavyojionea tumewapokea tisa pekee na hatufahamu wengine watatu waliko..”– Waziri Macharia.
Katika idadi hiyo ya watu tisa ni pamoja na watoto wanne na watu wazima watano ambao walikuwa kwenye ndege iliyotokea Brussels na abiria wengine 69 na majira ya saa 5:30 usiku wa jana.
Kuhusiana na Wakenya wengine watatu kati ya kumi na mbili waliotarajiwa kuwasili siku ya jana bado haijafahamika wapi walipo.
Waziri amesema serikali ina mpango wa kuwasafirisha kuwarudisha nchini humo Wakenya wengine watano kutoka Sierra Leone hivi karibuni.
Waziri ametangaza rasmi kuwa iwapo kuna mtu yoyote atabainika kuwa na dalili za Ebola atawekwa karantini kwa siku 21 na wale wasio na dalili zozote wataruhusiwa kurejea majumbani mwao.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook