Rapper Chidi Benz ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam baada ya kutimiza masharti ambayo ni pamoja na kupeleka Wadhamini wawili na shilingi milioni moja za Kitanzania ikiwa ni kutokana na kukamatwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege Dar akisafiri kwa Fastjet kuelekea Mbeya.