Amakweli duniani kuna mambo sikia hii… Mkazi wa kitongoji cha Itigi Mkoani Singida ameamua kumrejesha mkewe kwa wazazi wake akimtuhumu kuwa ni mvivu na mfujaji wa mali zake baada ya kushindwa kudhibiti kundi la fisi kushambulia na kuua ndama wa ng’ombe sita wakiwa machungani.
Mwanaume huyo aliamua kuchukua uamuzi huo juzi baada ya mkewe Hamida Simbe kurejea nyumbani akitokea kuchunga mifugo hiyo huku idadi ya ndama sita wakiwa wamepungua na ilipofika asubuhi alimtimua mkewe na kumtaka kurudi kwao.
Akisimulia kisa hicho katika gazeti la NIPASHE Baba mzazi wa mwanamke huyo aliyerudishiwa mwanaye alidai baada ya mtoto wake huyo kurejea kwa mumewe akiwa na mifugo pungufu alimweleza mumewe kuwa alivamiwa na fisi na ndama kuliwa lakini alipoambiwa hivyo alimtishia maisha mkewe na kumtaka arudi kwao.
Baba huyo alidai baada ya hatua hiyo alikasirika sana na hakutaka mkewe alale chumbani pamoja na mtoto wao mdogo na kulazimika kulala sebuleni hadi asubuhi aliporudi nyumbani kwa wazazi wake na kuwaambia hamtaki tena kwa sababu ni mfujaji wa mali zake hivyo anaomba apewe mke mwingine kutoka katika familia hiyo ili asirudishiwe mahari.
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Athuman Nkungu alisema Serikali ya kijiji hicho inafanya jitihada kuhakikisha inazikutanisha pande hizo zinazovutana ili kupata suluhu.