MTANZANIA
Polisi Mkoani Morogoro inamshikilia mwanamke mmoja Tausi Mohamed kwa tuhuma za kumjeruhi mtoto wa dada yake Jaffar Mashaka mwemye umri wa miaka11 kwa kumchanachana miguuni na mikononi kwa kutumia wembe kisha kumwagia chumvi kwenye vidonda hivyo kwa madai ya kumwibia shilingi 4500.
Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya Msingi Kiwanja Manispaa ya Morogoro alikutwa na majanga hayo majira ya saa12 asubuhi katika nyumba waliyokua wakiishi.
Mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni na Polisi kufuatia wasamaria wema kutoa taarifa na baadaye kukamatwa kisha kuhojiwa zaidi kufuatia tukio hilo kabla ya kufunguliwa mashtaka.
Mtoto huyo akisimulia kisa hicho alisema ilipofika asubuhi alichukua fedha hizo kwa ajili ya kununua chakua baada ya kuzidiwa njaa na ndipo mama yake huyo alipogundua na kumfanyia ukatili huo.
MWANANCHI
Watu watano wameuawa kikatili baada ya kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana kutokana na imani za kishirikina wakiwemo mume na mke.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Susan Kaganda alisema chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina na kwamba wauaji baada ya uhalifu walitoweka na juhudi za kuwatafuta bado zinaendelea.
Katika tukio lingine watu wasiofahamika walivamia nyumba usiku wa manane na kuua mume na mke ambao walikua wamelala.
Afisa mtendaji wa kata ya Bukoko Busambo Kanyerere alisema tukio hilo lilitokea na linadaiwa kuwa ni kulipiza kisasi kati ya wanakijiji na familia hiyo.
MWANANCHI
Katibu wa Bunge Dk.TBhomas Kashililah amesema kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali PAC chini ya Zitto Kabwe haikufuata utaratibu ilipoagiza kukamatwa na polisi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini TPDC Michael Mwanda na Mwenyekiti wake kwa kushindwa kuwasilisha mikataba26 ya gesi na mapitio yake mbele ya kamati hiyo tangu mwaka 2012.
Juzi viongozi wa TPDC walikamatwa na kupandishwa katika gari dogo la wazi la polisi na kupelekwa katika kituo kikuu cha Polisi lakini baadaye kupitia taarifa ya Suleiman Kova waliachiwa huru kusubiri sheria na taratibu za bunge.
Kashililah alisema utaratibu haukufuatwa kwa kuwa kamati ilitakiwa kumwandikia barua spika wa Bunge kuhusu suala ilo ili aweze kutoa maelezo kwa mwanasheria mkuu ambaye ndiye angeruhusu utarfatibu gani ufanyike.
Kauli ya Kashililah ilitofautiana na ile ya Zitto ambayo aliitoa juzi na kudai imetumia mamlaka yake ya kulazimisha maagizo yake kutekelezwa pale ambapo maofisa wa Serikali wanashindwa kutekeleza,PAC inamamlaka ya kuchukua hatua za kisheria kama ilivyofanya.
NIPASHE
Kutokana na Serikali kudaiwa zaidi ya bilioni90 na bohari kuu ya dawa ya Taifa MSD na kusababisha Hospitali nyingine kukosa dawa na wagonjwa kupoteza maisha,Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina ameomba Mkutano wa bunge ulioanza jana kuahirishwa ili fedha wanazolipwa wabunge hao zitumike kununulia dawa na kuokoa wagonjwa.
Naibu Spika Job Ndugai alisema suala hilo ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa na kutolewa uamuzi mara baada ya kikao hicho kumalizika.
Mpina aliomba mkutano huo kuahirishwa ili fedha walizopaswa kulipwa zikanunue dawa kwa ajili ya wagonjwa kwani MSD inaidai kiasi kikubwa cha fedha kwa muda mrefu sasa huku Watanzania wakiwa katika hali mbaya mahospitalini.
“Hatuwezi kupokea posho kila siku wakati ndugu zetu wako katika hali mbaya kwenye hospitali mbalimbali,naomba Bunge liangalie hili na ikiweza kuahirisha vikao hivi ili kuwaokoa wagonjwa”alisema.
MTANZANIA
Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umedai kunasa waraka wa Ofisi ya Rais Ikulu unaoonyesha Serikali imetenga bilioni2.5 kwa ajili ya kampeni ya kuwezesha katiba inayopendekezwa kupigiwa kura ya ndiyo
Katibu mkuu Wilbroad Slaa alisema jana kuwa kampeni hiyo itafanywa kupitia vyombo vya habari ili kuwahamasisha wananchi kuweza kupiga kura ya ndiyo ili kupitisha kwa urahisi katiba hiyo.
Waraka huo unadaiwa kutoka Ikulu kwenda kwa Wizara ya habari,Utamaduni na Michezo na kuelekeza kazi hiyo inatakiwa kuanza wiki hii zikipatikana milioni50 za kuanzia.
Alisema suala hilo ni kinyume na sheria kwa sababu wanaohusika na utangazaji au uhamasishaji wa katiba ni tume ya Taifa ya uchaguzi NEC na si ofisi ya Rais.
Alidai ofisi hiyo imendaa kamati ya kudumu ya habari kwa ajili ya kusimamia mpango wa kuelimisha umma hadi muda wa kura ya maoni utakapofika.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook