Ziara ya Rais Xi Jinping wa China iliyofanyika hapa nchini mwaka jana Machi imezua kizaazaa na kuitia ila sifa ya Tanzania kimataifa baada ya Maofisa waliokua wameambatana nae kuhusishwa na biashara haramu ya meno ya Tembo.
Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya kimataifa ya nchini Uingereza inayojihusisha na uchunguzi wa masuala ya mazingira inadai kuwa maofisa hao walinunua bidhaa hiyo kwenye soko la Mwenge jijini Dar es salaam kisha kuzisafirisha kidiplomasia kwa kutumia ndege ya rais huyo.
Taarifa hizo ambazo ziliandikwa na Gazeti la New York Times la Marekani na kuwa moja ya habari zilizopewa uzito mkubwa katika vyombo vingine vya habari ilipewa jina la ‘Ndege ya Rais kutumika kusafirisha meno ya Tembo’
Hata hivyo Katibu mkuu kiongozi Ombeni Semfue alisema kwamba Serikali haifahamu chochote kuhusu tuhuma hizo na kwamba hata kama zingekua na ukweli ndani yake waliopaswa kuulizwa ni Serikali ya China na si wao.
Baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari vya Kimataifa maofisa wa China walikanusha taarifa hizo wakisema hazina ukweli wowote.
MWANANCHI
Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam imesimamisha shughuli zinazofanywa na Polisi jamii baada ya kubainika kuwepo na vitendo vya wizi katika maeneo ya Kariakoo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wafanyabiashara wa Kariakoo kulalamika kwa Kamanda wa kanda hiyo Suleiman Kova kuhusu vitendo viovu vinavyofanywa na askari hao kwa kushirikiana na kituo cha Polisi Msimbazi.
Kova alisema kutokana na uhalifu huo Jeshi limeunda kamati ili kuwa na utaratibu sahihi wa kushughulikia kero za uhalifu na kuhakikisha kituo hicho kinakua imara na kutenda haki sawa kwa raia wote.
Alisema wanatarajia kufunga kamera zitakazosaidia jeshi hilo kutambua vibaka na majambazi wanaofanya uhalifu.
MWANANCHI
Mwanamke mmoja Mkoani Sumbawanga anashikiliwa na Polisi kwa kumuua mume wake kwa kumwagia maji ya moto kisha kuutumbukiza mwili wake mtoni.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Jacob Mwaruanda alisema tukio hilo lilitokea usiku wakati mumewe huyo aliporudi nyumbani na kuzuka ugomvi baina yao ndipo alipokimbilia jikoni na kuchukua maji ya moto kisha kumwagia usoni na tumboni hadi kufa.
Alisema kutokana na kukosa huduma ya kwanza mwanaume huyo alijikuta akipoteza maisha muda mchache baadaye na siku liliyofuata mwanamke huyo akishirikiana na wazazi wake waliuchukua mwili na kwenda kuutupa mtoni.
Alisema mpaka sasa Polisi inamshikilia mwanamke huyo kwa tuhuma hizo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
HABARILEO
Wizara ya Afya na ustawi wa jamii imeagiza Hospitali ya Taifa Muhimbili MNH kupitia upya mpango wao wa kupandisha gharama za matibabu,vipimo na chakula kisha kuwasilisha Wizarani kwa ajili ya mashauriano kuepuka kuwaumiza wananchi.
Aidha Wizara hiyo imesema imeandaa mwongozi wa kusimamia upandaji wa gharama za matibabu zikiwemo hospitali binafsi ili kuzuia upandishwaji holela wa gharama hizo.
Katibu mkuu wa Wizara hiyo Donan Mbando Wizara hiyo si tu inaandaa mwongozo kwa hospitali za Serikali bali utasimamia na hospitali binafsi lengo likiwa ni kuwapunguzia mzigo wa gharama za matibabu wananchi.
Aidha alisema Wizara hiyo itahakikisha tatizo la upungufu wa dawa linabaki historia na wameanza kuchukua hatua ikiwa kuiomba Serikali katika bajeti ijayo iongeze fedha za kutoka katika bohari kuu ya dawa ya Taifa MSD.
HABARILEO
Watu mbalimbali wakiwemo wageni katika Wilaya ya Nkasi wamefyeka na kuteketeza mti wa asili ujulikanao kwa jina la Mnyengwanyengwa kutokana na imani kwamba magome yake yanaongeza nguvu za kiume.
Mti huo uliopo kando ya barabara kimeupatia Mkoa wa Ruvuma sifa kubwa kwa wenyeji na wageni kutoka sehemu mbalimbali kuweza kujipatia dawa hiyo.
Baadhi ya wanakijiji walisema kuwa hatua za watu mbalimbali kukata mti huo zilianza miaka mitano iliyopita kwani ulikua mti mkubwa sana na sasa umebakia kisiki.
Mganga mkuu Wilaya ya Nkasi alisema katika mazingira ya kawaida ni vigumu kumzuia mtu kutumia dawa za asili za mitishamba kama ambavyo imekua ikifanyika katika jamii nyingi na wao kama wataalam hawana nafasi ya kumzuia.
NIPASHE
Mwanafunzi bora wa somo la hisabati katika mitihani ya Taifa ya darasa la saba iliyofanyika nchini mwezi Septemba mwaka huu,Rachel Kiunsi ameeleza siri ya mafanikio yake kuwa ni kujituma katika masomo na kuwaheshimu walimu.
Akizungumza jinsi alivyopokea taarifa ya matokeo yake Rachel alisema alipokea kwa furaha kubwa na alikua akitegemea kufaulu ila si kwa mafanikio kama hayo aliyoyapata.
“Ninamshukuru sana Mungu kwani nilikua namuomba anitendee maajabu katika matokeo yangu,nilikua ninasali kila nikianza na kumaliza mtihani,”alisema Rachel aliyekua akiishi na bibi yake Kimara Jijini Dar es salam.
Kwa upande wa mama yake mzazi akizungumza kwa simu kutoka Singida alisema matokea ya mwanaye aliyapata katika tovuti ya Mtihani na alifurahi sana ingawa hakujua kama mwanaye ameongoza katika somo la hisabati.
NIPASHE
Taasisi ya Moyo inakabiliwa na upungufu wa wataalam mbalimbali wa huduma hiyo nchini.
Akijibu swali la Mbunge wa Temeke Abas Mtemvu,Naibu Waziri wa uchukuzi Charles Tizeba alisema katia kukabiliana na upungufu huo wamekua wakiwapeleka madaktari watano kwenye mafunzo nje ya nchi kuchukua mafunzo ya uzamili katika fani ya upasuaji wa moyo.
Kuhusu wagonjwa waliopelekwa nje kutibiwa alisema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo jumla ya wagonjwa100 walipata rufani kwenda India kwa matibabu ya ugonjwa huo.
Alisema magonjwa hayo yanahitaji matibabu na utaalamu wa hali ya juu zaidi ambao kwa sasa haupatikani hapa nchini.
JAMBOLEO
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema nchi imefikia pabaya kwani Bunge limepoteza hadhi yake kwa wabunge kujadili porojo badala ya kujikita katika hoja za msingi.
Zitto alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge mmoja kusema baadhi ya wabunge wana akaunti za bilioni2 wakati wakilalamikia matumizi mabaya ya fedha za umma.
Alisema anasikitika kuona kwamba jumba tukufu limekosa hadhi na limegeuzwa la porojo,vioja halafu watu wanafurahia na kushangilia.
“Nchi inaeleka kubaya,kuna Mbunge hapa amesema kuna wabunge wenye akaunti za bilioni2,kikao hakiwezi kendelekea mpaka Mbunge aliyesema alete taarifa hapa ithibitishwe na ikiwezekana ashughulikiwe”alisema Zitto.
JAMBOLEO
Katika hali isiyokua ya kawaida mkazi wa Mbeya anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kuwauzia wenzake nyama ya mbwa kwa makusudi.
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmad Msangi alithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Ahadi Jesikaka mwenye umri wa miaka20 ambaye alidaiwa kuwauzia wateja wake nyama hiyo majira ya mchana.
Kamanda huyo alisema watu hao waliuziwa kitoweo hicho na kwenda kukitumia na baadaye kugundua kuwa ilikua ni nyama ya mbwa tofauti na walivyokua wakidhani.
Hata hivyo kamanda huyo amewataka wananchi kuwa makini hasa katika bidhaa kama hizo ili kuepuka kutapeliwa.
MTANZANIA
Walimu602 Mkoani Mwanza wamesema wataandamana iwapo deni lao la shilingi milioni153.3 halitalipwa na Serikali katika siku14.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu CWT Wilayani Kwimba Lameck Mahewa alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kutolipwa deni lao kwa muda mrefu sasa.
Alisema Walimu Wilayani humo wameafikiana kuandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya kushinikiza walipwe madai yao.
Mahewa alisema wametoa siku14 kuanzia Novemba5 kwa viongozi hao kushughulikia madai yao vinginevyo watafanya kile walichodhamiria ikiwemo kuandamana na kuendesha m gomo baridi wa kutofundisha wanapokua darasani.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook