Ni kawaida kuona Rais anaishi maisha ya kifahari ni jambo ambalo limezoeleka,hii ni tofauti kabisa kwa Rais Jose Mujica.
Rais Jose Mujica wa Uruguay ni Rais masikini zaidi Duniani anaeishi kijijini na anasifika kwa kuendesha gari lililochakaaVolkswagen Beetle ya waka 1987, huku akiishi maisha ya watu wa kawaida kubwa zaidi anatoa asilimia tisini ya mshahara wake huyapa mashirika ya misaaada ya kibinadamu na watu masikini.
Ni Raisi anaejulikana kama Raisi maskini Duniani kutokana na kuishi maisha ya umaskini wa hali ya juu.
Mujica alikataa kuishi maisha ya kifahari ambayo angegaramiwa na Serikali yake na badala yake amechagua kuishi kijijini yeye na mke wake, eneo ambalo ni nje ya mji lenye ubovu wa barabara na hana msaidizi yoyote na majukumu yote ya nyumbani anayafanya mwenyewe huku akiwana na ulinzi wa askari wawili tu.
Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari lake la Volkswagen.
“Naitwa Raisi maskini ila sijihisi maskini watu maskini ni wale wanaofanya kazi ili waisha maisha ya kifahari na siku zote wanahitaji kupata zaidi na zaidi” Mujiku
Rais Mujika anasema kuwa amepewa Dola millioni moja ili kuuza Gari lake aina ya Volkswagen ombi hilo lilitoka na kiongozi mmoja wa Dini ya Kiislamu katika eneo la Uarabuni.
Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini. Busqueda liliripoti kuwa ombi la gari hilo lilifanywa katika Mkutano wa Kimataifa mapema Mwaka huu katika Mji wa Santa Cruz Bolivia.
“Nilishangaa mara ya kwanza nikazarau lakini baadaye ombi jingine lilikuja na hivyo nikaanza kulichukulia kuwa swala la umuhimu” Mujik
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook