MWANANCHI
Hakufai..pengine ndio neno linaloweza kuleta uhalisia wa hali ilivyo katika baadhi ya hospitali za Serikali nchini,ambapo mamia ya wagonjwa wanateseka kutokana na uhaba wa dawa,vitendanishi na vifaa tiba ambavyo vimeendelea kuwa kikwazo.
Wengi wa wagonjwa waliohojiwa wanalalamika kushindwa huduma za gharama ambazo wanapaswa kuzinunua kwenye maduka wakisema hali hiyo inafanya maisha ya Watanzania wengi wenye kipato cha chini kuwa hatarini .
Kwa ujumla hali hiyo ni tofauti na matarajio ya wengi kwamba kungekua na mabadiliko hasa baada ya Serikali kutangaza kwamba imekwishalipa sehemu kubwa ya deni lililokua likidaiwa na bohari kuu ya dawa MSD.
Mbali na uhaba wa dawa na vifaa tiba, pia huduma ndani ya hospitali hizo hauridhishi hasa pale wagonjwa wanapokaa muda mrefu kati ya saa tatu hadi sita bila kupata huduma stahiki.
Katika Mikoa mbalimbali hali imekua ni mbaya na wengi wa wagonjwa wamedai huduma wanazopewa kwa sasa si za kuridhisha na ndugu zao wengi wamekua wakipoteza maisha na hali hiyo inayoonekana kutopatiwa ufumbuzi mpaka sasa.
MWANANCHI
Zaidi ya wanafunzi400 katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro wameshindwa kuendelea na masomo ya Sekondari kutokana na kukutwa na matatizo mbalimbali ikiwemo mimba na wengine kukimbilia katika biashara ya uchimbaji madini.
Ofisa Elimu Wilayani humo Ephraim Simbeye alisema Ulanga ni miongoni mwa Wilaya zinazoongoza kwa wanafunzi kuacha shule na inachangiwa na baadhi ya wazazi kushindwa kutoa taarifa sahihi za watoto wao licha ya Serikali kuendelea na jitihada za kuwatafuta na kuwafkisha katika mikono ya sheria.
Alisema utoro huo unazidi kukithiri siku hadi siku huku walimu wakikosa msaada wa wazazi katika kuhakikisha watoto hao wanarudi mashuleni na kuendelea na masomo.
Akizungumzia ujenzi wa Maabara alisema kwa sasa vyumba14 vimekamilika na vingine 54 vipo katika matengeneo ya hatua za mwisho kuweza kukamilika.
MWANANCHI
Naibu Katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba amesema viongozi wanaokimbilia kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kutaka madaraka wameishiwa kisera,kiimani na kwamba hawajiamini hivyo kamwe hawawezi kukubalika kwenye jamii na wasitegemee kupata nafasi wanazohitaji bila kumtanguliza Mungu.
Mwigulu ambaye ametangazania ya kugombea urais mw akani,ili kupata uongozi lazima umwamini Mungu kama yeye alivyowahi kuombewa wakati akitangaza nia ya kuwania ubunge wa Iramba Magharibi.
“Mimi wakati nagombea Ubunge nlmtanguliza Mungu kwa kuombewa na ndio maana nilifanikiwa,hivyo muda ukifika wa kuwania nafasi ninayoitaka nitafanya hivyo tena kwa kumshirikisha Mungu kwa sababu namuamini sana”alisema Mwigulu.
Alliongeza kuwa kwa wale viongozi wanaochanganya vjia mbili yaMungu na kwa waganda hawatafika mbali kwanihayo ni mambo ambayo hayawezi kuingiliana kama hawana sera kwa wananchi wao.
MWANANCHI
Bunge limeridhia azimio la kufuta na kusamehe madai au hasara itokanayo na upotevu wa vifaa na fedha za Serikali zaidi ya bilioni 10 kwa kipindi cha Juni30 mwaka 2011.
Kati ya fedha hizo kiasi cha bilioni4.9 kilitokana na hasara ya kuharibika kwa dawa zilizoingizwa nchini kwa ajili ya kurefusha maisha ya watu wnaoishi na virusi vya Ukimwi.
Hasara nyingine ni bilioni4.9 iliyotokana na kuungua kwa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hivyo kufanya hasara kubwa ya kiasi kilichoombwa kutokana na mambo hayo mawili makubwa.
Fedha nyingine zilitokana na kupotea vitabu katika shule mbalimbali nchini,ambavyo vimeshinndwa kurudishwa na wanafunzi.
Mwingulu alisema bunge limefanya uamuzi sahihi kufuta fedha hizo kwenye kitabu cha Serikali kwa kuwa hazilipi na fedha hizo hazikufanyiwa wizi bali kilichotokea ni hasara baada ya mali za Serikali kuharibika.
“Asilimia90 ya fedha zote tulizoomba zifutwe,inatokana na dawa zilizokwisha muda pamoja na kuungua kwa ofisi,hii ni hasara ambayo bado ingeendelea kutuharibia vitabu “alisema Mwigulu
NIPASHE
Serikali imeomba radhi kwa mauaji ya watu 17 ambayo yametokea Wilayani kiteto na imeahidi kupangua uongozi katika ngazi mbalimbali Wilayani humo na Mkoa wa Manyarakwa ujumla.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema Taifa limepoteza watu17 katika matukio yaliyotokea Wilayani humo kuanzia January hadi November kutokana na mapigano ya wakulima na wafugaji.
Alisema Serikali ya Kiteto itaimarishwa ili iweze kukabiliana na migogoro inayojitokeza kwa kufanya mabadiliko ya viongozi katika ngazi mbalimbali za utawala ndani ya Wilaya na Mkoa haraka itakavyowezekana.
“Naomba nitangulize kuomba radhi kwa vile matumizi ya silaha zilizotumika ni za kisasa na si za jadi kama ilivyozoeleka,hivyo hii ni aibu na inabidi vitendo hivi vionywe mapema kabla havijaleta madhara zaidi”alisema.
Pinda alisema mbali na hatua nyingine zinazochukuliwa kwa lengo la kukomesha matukio hayo,Serikali inaendelea kufuatili na kuangalia jinsi gani viongozi wataweza kutatua migogoro hiyo.
NIPASHE
Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangallah amesema wazee wakae pembeni kwa sababu zama zao zimekwisha kwnai safari hii ni zamu ya vijana kushikilia madaraka ya juu hapa nchini.
Msisitizo wa vijana kutaka kuwania nafasi ya urais ulitangazwa juzi na Mbunge huyo wakati wakati akizungumza na vijana wa CCM tawi la chuo kikuu cha ST.Agustin Mwanza.
Kigwangallah alisema lazima vijana wabadilishe tawira ya nchi kwnai wazee kuendelea kutawala watawadharau na kuwaona hawana dira ya maendeleo.
NIPASHE
Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali PAC inataraji kuwahoji Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema,Katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliachim Maswi,Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la umeme Tanesco Robert Mboma na wengine waliotajwa katika kashfa ya uchotwaji wa bilioni306 ya akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya benki kuu ya Tanzania.
Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kabidhiwa ripoti ya ukaguzi wa hesabu za akaunti hiyo na Naibu Spika Job Ndugai ili kufanyia uchambuzi na kutolea maelezo ya kina.
Baada ya kupokea ripoti hiyo Zitto alisema kamati itafanya kazi iliyokabidhiwa na ofisi ya spika kwa siri kwa kuwa ndani ya suala hilo kuna mambo ya mahakama hivyo wanaepuka kuingia katika malalamiko hapo baadaye ya mtu kuonewa na kwamba watahakikisha wanatenda haki.
Naye Mbunge Deo Filikunjombe alisema kamati yake ina uwezo mkubwa wa kumaliza shughuli hiyo ndani ya siku10 kuanzia sasa kwa kuwa kazi kubwa imekwishafanywa na CAG.
NIPASHE
Benki kuu ya Tanzania BoT imesema taasis za fedha zinatakiwa kuhakikisha mifumo yake ya fedha inakuwa imara na salama kwa wateja wake ili kupunguza wizi wa fedha kwa njia ya mtandao.
Aidha BoT imesema zoezi la kuhakikitaarifa za kibenki kwa wateja haliweze kusitishwa bali litakua endelevu.
Mkurugenzi wa usimamizi wa benki Agipit Kobello alisema BoT inahimiza benki kuhakikisha wakati wote zinakua na kanuni,taratibu na teknolojia mara za mawasiliano na mifumo ambayo ni ya usalama ili kuepusha wateja wake kutoka kwenye majanga.
Alisemakatika utekelezaji wa majukumu yake wa usimamizi wa mabenki,BoT imekua ikiwasiliana na benki zote kufuatilia mambo mbalimbali kiwemo ya usalama wa mifumo ya malipo.
Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na benki kufunga mitambo maalum ya kuzuia na kubaini wezi,kutunza kumbukumbu za matukio yoteya wizi,kuweka viooo vizuia risasi katika madirisha ya kuchukulia fedha na matawi yote ya benki kulindwa na walinzi wenye silaha za moto.
HABARILEO
Mchakato wa kuendelea kukabiliana na foleni katika jiji la Dar es salaam jana ulipata msukumo mpya baada ya kuwasili kwa kivuko kipya cha kisasa kinachokwenda kwa kasi zaidi kuliko vyote nchini cha Mv Dar.
Mbali ya Serikali kuahidi kuleta kivuko hicho pia imekua ikiboresha barabara zake kuwezesha magari yaendayo kasi ,lakini pia imekua ikipanua kwa kiwango cha hali ya juu barabara zake katika Manispaa tatu Jijini Dar es salam.
Kivuko hicho kilipokewa jana na Waziri wa Ujenzi John Magufuli ambaye alisema ujio wake ni juhudi za Serikali katika kukabiliana na foleni.
Alisema kivuko hicho kmegharimu kiasi cha bilioni7.9 na kitaanza kutumika hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa mwisho,ambapo pia aliwataka wananchi kushiriki katika kukilinda.
Alisema kivuko hicho kabla ya kuingia nchini kilikaguliwa na Mamlaka ya majini na nchi kavu Sumatra,ujenzi pamoja na TEMESA ili kuhakikisha kinakidhi mahitaji lakini pia kitafanyiwa majaribio tena baada ya kuwasili.
MTANZANIA
Vita dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa UKIMWI huenda ikaingia dosari baada yamfuko wa dunia wa kupamba na ugonjwa huo,kifua kikuu na Malaria (Global Fund) kutishia kuinyimaTanzania msaada wa bilioni328.793.
Hatua hiyo inakuja baada ya Serikali kuomba zaidi ya dola milioni400 kutok katika mfuko huo kwa ajili ya mapambano dhidi ya magonjwa hayo mwaka wa fedha 2015/16
Wahisani hao wamekataa kutoa takriban trilion moja wakiitaka Serikali ichukue hatua dhidi ya sakata la kampuni ya kufua umemeya IPTL lililosababisha upotevu wa zaidi ya biloni200 katika akaunti ya Escrow.
Mwenyekiti wa hisani katika shughuli za Ukimwi Dk.Mishelle Rowland alisema fedha zilizopo ni kidogo na kushauri kiasi kilichopo kikaelekezwa katika maeneo ambayo yataleta tija kama vile kwa watoto wadogo,wasichana,wanawake na makundi maalum.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook