Vitu vingi sana sasa hivi ukichunguza ni biashara, ni siku tu zimepita toka Mtanzania Feza Kessy alietuwakilisha kwenye mashindano ya Big Brother Africa 2013 aliposema kazi yake nyingine kubwa anayoifanya Afrika Kusini ambayo inalipa pia ni kualikwa kwenye matukio mbalimbali, yani ile kuonekana kwake tu analipwa sababu ni staa.
Tukiachana na hiyo, kuna rafiki yangu kwenye twitter saa kadhaa zilizopita aliuliza swali ambalo limenipa stori kuhusu zile mechi za kirafiki ambazo Taifa Stars imekua ikicheza na timu maarufu za mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Brazil.
Kama ulikua unajua huwa wanakuja kucheza bure utakua uko kwenye njia isiyosahihi….. Rais wa TFF Jamal Malinzi alimjibu Remija kwenye twitter baada ya kuuliza <<< Hivi ule utaratibu wa kucheza mechi za kimataifa na timu kubwa uliishia wapi? mfano Brazil, Ivory Coast, SA, Misri n.k <<<<<
Rais Jamal Malinzi aliwamjibu >>> ‘Taratini za maandalizi yake na hata malipo ni ngumu, timu kubwa zinadai pesa ya kuonekana hata dola milioni mbili’ ni pesa ambayo kibongobongo inagonga kwenye 3459000000
@jamalmalinzi Mh hivi ule utaratibu wa kucheza mechi za kimataifa na timu kubwa uliishia wapi?Mfano Brazil,Ivory Coast,SA,Misri etc
— Simba Kapakatwa Pub (@1960Remija) November 19, 2014
@1960Remija Taratini za maandalizi yake na hata malipo ni ngumu.Timu kubwa zinadai appearance money hata dola milioni mbili — Jamal Malinzi (@jamalmalinzi) November 19, 2014
@jamalmalinzi Hizo ni za Afrika au nje ya Afrika?Kama sio,tunaweza kuomba hata kwa walio top 10 kwenye ubora Afrika. Wadhamini hawawezi?
— Simba Kapakatwa Pub (@1960Remija) November 19, 2014
“@1960Remija:Kama sio,tunaweza kuomba hata kwa walio top 10 kwenye ubora Afrika. Wadhamini hawawezi?” toka top 10 africa inawezekana — Jamal Malinzi (@jamalmalinzi) November 19, 2014
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook