Wiki moja baada ya Nahodha wa Meli iliyozama kuhukumiwa kifungo cha miaka 36, na wenzake 13 hukumu ya miaka 30 kila mmoja, kumbe kuna watu wengine ambao wana hatia kutokana na kupatikana na hatia ya uzembe uliopelekea meli kuzama na kuua watu 300.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayomiliki Meli hiyo ya Mv. Sewol, Kim Han-Sik, amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuruhusu meli hiyo kupakia mizigo kuzidi uwezo wake.
Mbali na mkurugenzi huyo, wengine 9 wamehukumiwa miaka 6 kila mmoja na mmoja kati ya watuhumiwa ameachiwa huru kwa kukutwa bila hatia.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook