Kama haukusikiliza ama kutazama Kikao cha Bunge Dodoma leo, moja ya masuala yaliyotawala ni kuhusu Mamlaka ya Bunge na Mahakama, wa kwanza kuzungumza alikuwa David Kafulila; “… Naomba mwongozo kuhusiana na taarifa ya PAC kuhusiana na sakata la ufisadi wa ESCROW kama italetwa ama haitaletwa na msingi wa swali lile ulikuwa ukizingatia kwamba zimekuwepo taarifa za mkakati wa kuhakikisha Mahakama inatumika kuhakikisha ripoti ile hailetwi Bungeni na kufikia mwisho…”
“…. Kwa kuwa suala hili ni suala nyeti, Watanzania wote wanafuatilia jambo hili kwa umakini kujua hatma ya jambo hili naomba Mheshimiwa naibu Spika utupatie mwongozo wa Bunge na Watanzania kuhusu uhakika wa Ripoti hii kuletwa Bunge hili ili kuondoa mashaka ambayo yamekuwa yakijengeka kwamba kuna mikakati.. kuna njama ambazo Mahakama inataka kutumika kama kichaka cha kuweza kuficha wezi wa hizi fedha, na kwa hiyo Watanzania.. ili kusudi Watanzania waliamini Bunge lako tukufu kwamba ndiyo ‘Supreme organ’ kwenye uendeshaji wa nchi hii na kwamba jambo hili litajadiliwa katika Bunge hili na tutafanya maamuzi ya mwisho…“– David Kafulila.
“…Lakini vilevile Watanzania wafahamu kwamba sio tu kwamba Mahakama haipaswi kuingiliwa na Bunge lakini pia Mahakama haipaswi kuingilia Bunge. Ningeomba uhakikishie Watanzania kuhusiana na jambo hili kwa sababu majibu ya Waziri Mkuu yalikuwa nusunusu hayatoi uhakika kwamba Ripoti hii italetwa au haitaletwa…”– Kafulila.
Naibu Spika Job Ndugai akajibu; “… Asante sana, nitatolea mwongozo jambo hili mwishoni…”
Baada ya hapo akateuliwa Mbunge Esther Bulaya, ambapo kutokana na mwongozo alioutoa ulikuwa sawa na wa Mbunge Kafulila akaombwa asubiri ili wachangie wengine, mwongozo kuhusu ESCROW ungehitimishwa mwisho wa kikao hicho.
Naye Moses Machali alipewa nafasi akasema haya; “… Ukifanya ‘situational analysis’ ya mwenendo wa Bunge letu hivi sasa, Bunge limegubikwa na kupuuzwa na kudharauliwa na mihimili mingine ikiwemo Serikali na sasa Mahakama nayo imeanza ku-penetrate kwenye kudharau hili Bunge…”
“… Suala langu ni nini.. Unadhani Wabunge ambao pengine tungependa kuona haki, kinga na madaraka ya Bunge hayaporwi, tufanye nini au tutumie nguvu gani za ziada ili kuweza kudhibiti Mihimili mingine ambayo imekuwa inataka kupora uhuru na Madaraka ya Bunge kama ambavyo imeainishwa kwenye Ibara ya 100… kama hili suala ambalo ESCROW leo hii linatikisa…”– Machali
Kama hukupata nafasi ya kusikiliza mjadala huo wa Bunge Leo Novemba 20 unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play hapa.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook