Huenda umekuwa mbali na vyombo vya habari kufahamu kilichojiri Bungeni leo Novemba, uhali ya mazingira ya Dar imezungumziwa, unajua ahadi aliyoitoa Waziri Aggrey Mwanri?
Wa kwanza kuuliza swali alikuwa Anne Kilango; “…Iwapo Serikali iliaweza kusafisha jiji la Dar es salaam likawa safi kuzidi hata Geneva wakati alipokuja Rais Obama pale Dar es salaam inashindwaje sasa kumaintain hali ile ikaendelea kuweka jiji la Dar es salaam katika sura inayopendeza na kuvutia watu wote wanaokuja Dar es salaam.“
“..Kariakoo ni kitovu cha biashara ya jumla kwa Afrika Mashariki wanakuja wafanyabiashara wa Kenya, wa Uganda na wafanya biashara wote wa Tanzania wanakuja Kariakoo kwa ajili ya kuchukua biashara kwa jumla, lakini mheshimiwa mwenyekiti miundombinu ya jiji eneo la Kariakoo sio rafiki kwa biashara, hivi Serikali haioni ni aibu kwamba Afrika mashariki wote wanakuja kununua kwa ajili ya Kariakoo lakini imeshindwa kutengeneza miundombini ya Kariakoo?”- Anne Kilango
Aggrey Mwanri; “.. Nidhamu maana yake ni kufanya jambo kama linavyotakiwa, kwa wakati unaotakiwa na mahali linapotakiwa , kama Mheshimiwa Rais Obama alikuja hapa tukasafisha mji ukawa msafi maana yake kulikuwa kuna discipline tulipeleka pale ndio maana tukaonekana kama tulivyooonekana..“
Kilichofanyika Mheshimiwa kwanza kilifanyika kitu kinachoitwa Sheria ndogo, mtu akifanya hivyo anatozwa shilingi elfu hamsini kama ikitokea hivyo, Moshi kimefanyika kitu kama hiki tunachozungumza Mheshimiwa Mwenyekiti na pale Moshi ndio ipo hiyo discipline, mtu akikwangua Vocha akamaliza akatupa Barabarani wanamdaka pale pale..“– Aggrey Mwanri.
“..Ninachoelewa hapa mheshimiwa mwenyekiti ni kweli kama anavyosema mheshimiwa Anne Kilango kwamba kumekuwa kuna nini, ni kwamba sisi tunakiuka taratibu sisi wenyewe, tumemtuma Katibu Mkuu wa Wizara ya kwetu ndugu Sabini, amekwenda mpaka Dar es Salaam, amewachukulia hatua watendaji wote wanaohusika na mambo ya uchafu hapa, nimesema na ninasema maneno haya kwa sababu nataka mheshimiwa msinihukumu kwa jambo hili kama halikufanyika, sasa mimi naulizwa hapa nijibu swali na najibu swali sasa nasema sasa sindio nimemuambia katibu mkuu wa wizara aende pale akasimamie jambo hili kwa hiyo tumefanya hilo jambo hiyo ndio hatua ambayo tumechukua…“– Aggrey Mwanri.
“..Lakini mimi nasubiria maelekezo hapa nikipewa maelekezo hapa mimi bado nitaendelea kufanya hivyo kwa sababu mimi ndo ninayetakiwa kusimamia kazi hiyo..
Kuhusu Kariakoo ni kweli kama unavyosema Mheshimiwa ni kweli na hela zinazookotwa pale ni hela nyingi za kutosha, no hakuna mtu anaetaka kuiona Kariakoo ikaonekana kama inavyooonekana, pale palikuwaga na jitihada za kuondoa Magari pale sasa hivi at least magari yanaweza kukimbia pale, lakini I’m saying katika hii jitihada ambayo nimesema hapa, Mheshimiwa hiyo najua kitu hiki ninachozungumza hapa ni sensitive mimi napokea maelekezo haya na nataka nikuambie kwamba, tutaendelea kusimamia kuhakikisha kwamba hali hii inaondoka, pale lipo jiji, zipo na manispaa hizo ambazo nimesema hapa tutazisukuma tuhakikishe kwamba jiji la Dar es salaam linakuwa katika hali ya usafi kama wanavyosema waheshimiwa wabunge…“– Aggrey Mwanri.
John Mnyika; “.. Mheshimiwa Naibu Waziri hajajibu swali aliulizwa swali ni kwanini Rais Obama alikuja jiji likawa safi kwa nini sasa hivi Serikali inashindwa kufanya jiji liwe safi? sasa naomba kuuliza swali la nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri amesema hapa kwamba, katibu mkuu wa Wizara amekuja Dar es salaam na amewachukulia hatua watendaji wote amesema neno wote wanaohusika na usafi, mimi nina taarifa za watendaji ambao wanakusanya fedha za wananchi lakini usafi wa mazingira haufanyiki kwenye mitaa, anaposema kwamaba watendaji wamechukuliwa hatua atutajie ni watendaji gani? Wakati bado watendaji wengi wanasimamia uchafu badala ya kusimamia usafi?..“
Aggrey Mwanri; “..Kwanza nataka nilieweke vizuri habari ya wote ni yeye amesema hapa habari ya wote, sasa kama si napata nafasai ya kuzungumza hapa ili ni clarify? Afadhali nilinde tuu mzee wangu mi naomba unilinde hapa, ninachosemaa wale ambao tulibaini kwamba wanamatatizo hatua hii mheshimiwa mwenyekiti sio hatua ndogo, kama hatua levo ya wizara tunaweza kumuagiza mtendaji mkuu aende Dar es salaam na akapita na akafanya ziara, ambayo najua kabisa wewe Mheshimiwa huku dispoti na yeye Mheshimiwa Mnyika hakudispoti ni kweli wale ambao tulibaini wanafanya hivyo tuliwachukulia hatua..“
“..Mimi Mheshimiwa nisibishane na kiti chako niseme kwamba presha hii naiona naipokea hii changamoto niyakwangu mimi kwa sababu ndio msimamizi wa jambo hili, mimi nitakwenda kuchukua hatua zote zinazotakiwa na mi nitahamia hapo Dar es Salaam, nikihamia Dar es salaam itakuwa ni vurugu tuu..”– Aggrey Mwanri.
Kama unahitaji kusikiliza kilichoendelea wakati wa mjadala huo unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play hapa.