Leo Novemba 22 taarifa ya habari iliyoripotiwa na kituo cha ITV inahusu kuvuja kwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG kuhusiana na kashfa ya wizi wa fedha zaidi ya bilioni 300 kwenye akaunti ya Escrow imekutwa inasambazwa mitaani.
Ripoti hiyo imekutwa ikiwa imetolewa karatasi tatu za mwisho muhimu ambazo zina majina ya wahusika waliogawana pesa hizo kwa lengo la kutengeneza propaganda ili kuwadanganya wananchi kuwa taarifa hizo hazijawataja wahusika.
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia amesema; “… imenyofolewa zile karatasi tatu ambazo ni muhimu zile za mwisho ambazo ndio zinatoa hitmisho la uchafu wote uliofanyika.. Baada ya kutoa zile kurasa tatu za mwisho, wakachukua taarifa hii kwa namna walivyoipata wanajua wao wenyewe na kuanza kuisambaza kama njugu.. PAC wamejifungia wanasema ni taarifa ya siri lakini taarifa iko mitaani.. Sisi kambi ya upinzani Bungeni tumeona ni jambo baya sana, ni jambo ovu, ni jambo la kifisadi, ni jambo la kishetani wanalotaka kuliingiza taifa letu liigie kwenye machafuko kwa ajili ya maslahi ya watu wane, watano, sita, saba… Baadhi ya watuhumiwa wameshakamatwa wako mikononi mwa jeshi la Polisi…”
Naye Mjumbe wa UKAWA John Mnyika amesema; “… Rai yangu kwa Jeshi la Polisi watuhumiwa hawa ambao wamekamatwa na hasa mmojawapo wa watuhumiwa ambaye naamini Jeshi la Polisi litapaswa kumtaja kwa jina na kadhalika… Mimi ninazo taarifa kwamba mtuhumiwa huyu ana mahusiano ya karibu na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.. Kama mmoja wa watuhumiwa ana mahusiano na Sospeter Muhongo ambaye ni mmoja wa watuhumiwa nahitaji vilevile Jeshi la Polisi linapowahoji watuhumiwa waliokamatwa hasa huyo mtuhumiwa mmoja wao lichunguze vilevile mahusiano ya mtuhumiwa huyo na Sospeter Muhongo …”
Katibu wa Bunge Thomas Kashirira na Kamanda wa Polisi Dodoma wamesema wamesikia kuhusu taarifa hizo na wanazifanyia kazi ili watoe taarifa rasmi.
Taarifa hiyo kutoka ITV iko hapa unaweza kuisikiliza.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook