Ugonjwa wa Ebola umeendelea kuwa tishio hasa nchi za Magharibi mwa Afrika na kuendelea kuua maelfu ya watu.
Pamoja na jitihada mbalimbali kuchukuliwa na nchi nyingi za kiafrika kwa ajili ya kupambana nao zikiwemo za Bararani Ulaya lakini nchi za Magharibi bado zimeendelea kupoteza watu kutokana na ugonjwa huo.
Raia mmoja nchini Nigeria Yemi Oyekoya ameamua kuhamasisha watu kuchangisha fedha ilikusaidia waathirika wa ugonjwa huo pamoja na kutoa elimu ya jinsi virusi vya ugonjwa huo vinavyoweza kuenea kwa kutumia baiskeli yake kutoka Nigeria hadi nchini Ghana.
Amesema anatarajia kuanza safari hiyo mapema mwezi wa kwanza mwakani na safari hiyo itakua ya zaidi ya kilomita100
”Lengo langu ni kuweka ufahamu zaidi wa kupambana na ugonjwa uliozikumba baadhi ya Nchi za Afrika Magharibi, juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola mapambano ambayo yanawezekana kufanywa kwa hiari kwa mchango wa Serikali, Sekta binafsi, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na watu binafsi.
Nina shauku ya dhati kupambana na Ebola hivyo nahitaji kutumia Baiskeli yangu kufikisha ujumbe na kujenga uelewa zaidi
Baiskeli inanipa shauku ya kusafiri ambayo nitaitumia kusafiria Nchi tofauti toka mwaka 2007, kwa upande wangu napenda Baiskeli na napenda kusafiria Nchi tofauti wakati mwingine inanipa furaha kubwa hasa pale ninapoona Nchi tofauti na tamaduni tofauti.
Nataka kuwatia moyo juu ya hiki kitu kipya kwa kila mtu na changamoto za safari, nataka kutumia hizi jitihada kuunganisha kila mtu juu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa ebola uliozipata Familia, Wafanyakazi, na hasa watoto wengi kuugua”
Hayo ni maneno yaliyosemwa na Yemi Oyekoya, kijana kutoka Nigeria ambae ameahidi kufanya matembezi ya kupanda zaidi ya kilomita 1000 na mile 600, safari ambayo ataianzia Ghana mpaka Nigeria kukusanya hela kwa ajili ya mapambano dhidi ya virusi vya Ebola.
Akiongea na News Agency of Nigeria (NAN) Yemi amesema safari hiyo anaitumia kujenga uelewa zaidi kwa mapambano dhidi ugonjwa a Ebola na kuwasaidia waathirika.
Ni ahadi yangu kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook