Leo Desemba 01 ilikuwa siku ambayo ilipangwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili msanii Chid Benz.
Kesi hiyo imeahirishwa kwa mara nyingine tena kutokana na ushahidi wa upelelezi kutokukamilika ambapo kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka Desemba 04 mwaka huu.
Hata hivyo Chid Benz hakufika Mahakamani japo aliwakilishwa na wadhamini wake wawili waliomuwekea dhamana.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook