Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema wizi wa bilioni 306 kwenye akaunti ya Escrow ni matokeo ya nchi kuwa na Katiba isiyo na vifungu vinavyozungumzia mambo hayo.
“.. Katika mchakato wa Katiba Mpya tulisema kuwe na mgawanyiko wa madaraka na kila mtu ajue madaraka yake ni nini na kutenganisha Serikali na Bunge…”
“… Kama Serikali na Bunge vingetenganishwa na Bungeni usingeibuka mvutano kuhusu waliochota fedha za Escrow. Bunge lingekuwa huru katika utendaji wake wa kazi…”
Alitaja Ibara ya 19 iliyokuwa katika Rasimu ya Katiba ambayo imeondolewa katika Katiba inayopendekezwa anayosema; ‘ Kiongozi wa umma hataruhusiwa kutuhumiwa au hataruhusiwa kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya umma, zikiwamo zilizokodishwa kwa Serikali, kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi au kumpatia mtu mwingine kwa manufaa yoyote…”
MWANANCHI
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya Profesa Mussa Assad ameapishwa jana Desemba 02 na kuahidi kuanza kazi kwa moto sawasawa na ulioachwa na Mkaguzi aliyestaafu, Ludovick Utoh.
Mkaguzi huyo ameahidi kuisimamia Serikali na kulinda hadhi na heshima ya ofisi hiyo, aidha amesema anasubiri kukabidhiwa rasmi taarifa ya Ripoti ya Escrow ambayo ina taarifa ya maazimio ya Bunge ili aanze kuyafanyia utelezaji wa yale yalioagizwa katika Ripoti hiyo.
Mstaafu wa nafasi hiyo, Ludovick Utoh amesema amemkabidhi Prof. Assad ofisi ambayo ina watendaji wanaofanya kazi kwa ari na ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na kumkabidhi mwongozo maalum wenye kurasa 78 ambao una mwongozo wa utendaji wa ofisi hiyo na yuko tayari kushirikiana naye wakati wowote.
Spika wa Bunge Anne Makinda amemwambia CAG Assad kwamba kashfa ya Escrow imelifanya Bunge kujenga misingi mizuri zaidi kiutendaji na uwajibikaji katika kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.
NIPASHE
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimemtaka Naibu waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuwapatia shilingi bil. 16 kutoka kwenye pesa za Escrow ili watatue changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Ezekiel Ulouch amesema kiwango hicho cha pesa kitasaidia kutatua changamoto kadhaa ikiwemo ya ukosefu wa madawati, kutekeleza muundo mpya wa walimu na kuboresha mazingira ya shule.
TANZANIA DAIMA
Wanaume wawili katika Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe wamefumaniana na kulazimika kubadilishana wake zao baada ya kufanya makubaliano ya maandishi yaliyosimamiwa na Serikali ya Kijiji.
Afisa Mtendaji wa Kijiji ambapo limetokea tukio hilo amesema watu hao Paul Mboma alikutwa na Nuru Sangwela, Ambakisye Mwakasege alikutwa na Lusie Lusepo ambapo kila mmoja alikutwa na mke wa mwenzake na chini ya usimamizi wa Mtendaji huyo wakakubaliana kubadilishana ambapo kila mmoja alimchukua mke wake na wakasaini makubaliano hayo.
Wamesema kuwa maafikiano hayo yamefikiwa ili kuepusha urafiki wao usiharibike.
TANZANIA DAIMA
Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili Aboubakar Aman na Ezekiel Kasenegala kwa mauaji ya wasichana wawili ambapo imesemekana wamekuwa wakiwalaghai kimapenzi na kuwawekea dawa za kulevya kwenye vinywaji, na kasha kuwabaka na kuwaua.
Wasichana waliouawa walikuwa wasichana hao ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Ukutubi cha Bagamoyo, Wenze Makongoro na Jackline Masanja na miili yao kutupwa katika maeneo tofauti Dar.
Kamishna wa Polisi Suleiman Kova amesema watuhumiwa wamekutwa na nguo, hereni, mikoba na simu ambapo vyote vilikuwa vinamilikiwa na marehemu hao.
Taarifa kuhusu vifo vya wasichana hao iliwahi kuripotiwa na kituo cha Redio Clouds Fm wiki iliyopita katika kipindi cha Hekaheka.
UHURU
Mafundi uashi wawili wamegundua mabomu manane ya kutupwa kwa mkono ambayo inasemekana yamekuwepo ardhini kwa Zaidi ya miaka 10 Kigoma kwenye Kijiji cha Mabamba walipokuwa wakichimba msingi wa nyumba ya Mganga wa Kituo cha Afya.
Mafundi hao wamesema baada ya kubaini kuwepo kwa chuma ambacho hawakukitambua waliamua kuoa taarifa Polisi na Jeshi la Wananchi JWTZ, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed amethibitisha kutoa kwa tukio hilo.
Kamanda huyo amesema wanaendelea kuwahoji wayu kadhaa ikiwemo Diwani wa wa Kata hiyo ambaye alikuwa anaimiliki nyumba hiyo kabla ya kuiuzia Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto amesema huenda mabomu hayo yaliachwa na wapiganaji wa kutoka Burundi walipokuwa nchini kama Wakimbizi.
Ni ahadi yangu kukufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook