Tumesikia visa vingi ikiwemo vile vya kujiua ama kujidhuru kwa namna yoyote ambavyo vinasababishwa na mikasa ya mapenzi, kila kukicha tunasikia kisa ama visa vipya ambavyo watu wanajikuta wakijitenda kutokana na masuala ya mapenzi.
Oliver Ilic ambaye ana umri wa miaka 23, leo kaingia kwenye orodha ya watu ambao wamewahi kujidhuru kutokana na masuala ya kutendwa kwenye mapenzi huko Macedonia.
Oliver alijikata sehemu zake za siri na kutupa katika kapu la kuwekea taka lililopo chumbani kwake, ambapo alifanyiwa operation ya kuzirudishia japo madaktari hawakuweza kutoa majibu kama jamaa huyo ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida.
Jamaa huyo amesema aliamua kujikata baada ya mpenzi wake kumwambia kuwa hana jipya kitandani.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook