Wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika ligi kuu msimu huu Chelsea leo wamejikuta ndoto zao za kumaliza msimu bila kufungwa zikipotea.
Hii ni baada ya kupokea kipigo cha 2-1 kutoka Newcastle, timu ambayo Jose Mourinho hajawahi kuifunga katika uwanja wake wa nyumbani tangu alipowasili England kwa mara ya kwanza mpaka leo hii.
Magoli ya msenegali Papiss Cisse yalitosha kulizamisha jahazi la Chelsea ambao leo walimkosa mchezaji wao muhimu sana Nemanja Matic.
Didier Drogba aliifungia Chelsea goli la kufutia machozi.