Mwanaume mmoja mkazi wa Shinyanga amemshambulia mkewe kwa nondo kichwani kutokana na itikadi ya vyama vya siasa.
Inadaiwa alifanya hivyo kutokana na kunyimwa kuuza chakula cha familia ili uemdesha kampeni kwa ajiliya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, upigaji kura, kuchagua wenyeviti wa mitaa na vitongoji utakaofanyika Jumapili Desemba14 mwaka huu.
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari limefungua jalada huku likimsaka mtuhimiwa ili aweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Mkewe anayetambulika kwa jina la Theresia Dotto ambaye ni mwanachama wa CCM huku mumewe akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Mtaa kupitia Chadema akizungumza kwa taabu Hospitali alisema alimkataza mumewe kuuza chakula cha familia na mumewe kukasirika na kuamua kumpiga huku akihoji kwa nini anamzuia kuuza mpunga.
“Mara ya kwanza mimi alinificha akaenda tunaputunzia mpunga na kuuza debe mbili na fedha alizopata alikwenda kuwalipa mawakala wa chama chake waliokua wanasimamia uandikishwaji”alisema mwanamke huyo.
HABARILEO
Katika jamii watu wengi wanathaminika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwa na fedha alizonazo ama madaraka anakofanyia kazi,eneo alipo au mahali anapoishi.
Kwenye maeneo mengi fedha ni chimbuko la heshima na ndio maana hata mtu akiwa mdogo lakini ana pesa nyingi ni lazima ataheshimika na kupendwa katika jamii.
Kwa Sumbawanga hali ni tofauti kwani huheshimiwi kwa sababu ya fedha zako ila kutokana na idadi kubwa ya watoto uliowazaa.
Mkazi wa kijiji cha Chitete,Sumbawanga anatamba kuwa anaheshimika na kuitwa mzee kwa sababu tu amezaa watoto14 na ana wanawake wawili ambapo kila mmoja amemzalia watoto saba.
“Ni heshima sana mbele ya wanaume wenzangu kuwa na watoto 14,ninaitwa mzee kwa ajili hiyo lakini sasa tunatumia njia za uzazi wa mpango baada ya kuelimishwa lakini tayari nimezaa watoto wote hawa,mimi sijasoma lakini watoto wangu wote wanasoma,saba wapo Sekondari”alisema.
MWANANCHI
Ikiwa kesho ni mwisho kwa Mikoa kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa Maabara kwa shule za Sekondari nchini,baadhi ya Mikoa imetekeleza agizo hilo kwa asilimia 95 wakati mingine imetimiza kwa asilimia kati ya 30 na 50 na mingine ina asilimia sifuri.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo akiwataka Maofisa elimu wa ngazi mbalimbalikuhakikisha kwamba kilashule ya kata inakua na Maabara mbili na kurejea agizo hilo mwaka huu akisisitiza kuwa ujenzi huo utakamilika Desemba9.
JK alisema ifika Novemba30 mwaka huu anataka kuona vyumba vya Maabara vimekamika,hata hivyo aliongeza muda hadi Disemba9.
“Nitawawajibisha wakurugenzi watakaoshindwa kukamilisha ujenzi wa Maabara ifikapo siku hiyo,sitakua na mzaha”alisema Kikwete.
MWANANCHI
Wakati vyama vya siasa vikitafakari jina la mgombea urais,Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila tayari anaye mtu anayefaa ambaye ni Dk Wilbroad Slaa.
Kwa maoni yake,si kwamba viongozi ama wanachama wa vyama vingine vinavuounda Ukawa hawana sifa za kuwania nafasi hiyo ya juu katika siasa ya nchini,bali Dk Slaa ana sifa ya ziada pamoja na mvuto.
Miongoni mwa watu wanaopewa nafasi ya kuteuliwa kugombea Uraiskwa tiketi ya Ukawa ni pamoja ba Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba,James Mbatia,Freeman Mbowe na Dk Slaa.
“Ni mapema mno kusema kama Ukawa inaweza kushinda au vinginevyo,inategemea tunajipangaje,tukifanya makosa tutashindwa vibaya,makosa ya CCM naUkawa yanategemeana kwenye kuamua nani agombee”alisema Kafulila,
Alisema Rais mwenye uweledi ataweza kuchambua kila ushauri anaopewa na kwamba kama nchi itakua na Rais asiye na weledi ni rahisi kupokea ushauri mbaya kutoka kwa watu na kulisisitiza.
MWANANCHI
Rais Kikwete amempandisha Cheo Mkuu wa Wilaya ya Karatu Daudi Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuwahamisha wakuu wengine wa Mikoa sita kuanzia jana.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu mkuu wa Ikulu Omben Sefue ilisema kuwa Ntibenda ataapishwa leo saa nne asubuhi Ikulu.
Wakuu wa Mikoa waliohamishwa ni pamoja na Elaston Mbwilo kutoka Manyara kwenda Simiyu,Joel Bendera kutoka Morogoro kwenda Manyara,Magalula Magalula amehamishiwa Tanga aitokea Lindiambako nafasi yake itazibwa na Mwantumu Mahiza kutoka Pwani.
Evarist Ndikilo amehamishiwa Pwani akitokea Arusha alikohamia hivi karibuni akitokea Mwanza.
KatikaTaarifa hiyo Sefue alisema Wakuu wa Mikoa wengine wataendelea kubaki katika vituo vyao vya kazi.
Uhamisho huo umekuja ikiwa ni mwezi mmoja tangu Kikwete afanye mabadiliko mengine ya wakuu wapya wanne wa Mkoa na kuwahamisha sita huku wengine watatu wakipangiwa kazi nyingine.
MWANANCHI
Katibu Mwenezi wa Chadema kata ya Rigicha Wilayani Serengeti Bahati Mayala amelazwa katika hospitali teule ya Nyerere baada ya kujeruhiwa na mshale wakati akitoka kwenye kampeni.
Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Calvin Mwasha alikiri kumpokea majeruhi huyo akiwa na mshale mgongoni majira ya saa 6 usiku na kufanyiwa upasuaji kutoa silaha hiyoya jadi.
Mwasha alisema mshale huo uliinia nchi sita katika eneo la mapafu huku mwenyewe akisema alipigwa baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Nikiwa njiani wakati narudi nyumbani nilisikia kinakita mgongoni kwa nguvu…nikaona watu wawili wanakimbia ambao niliwafahamu kutokana na mavazi yao waiyokua wamevaa na majina yao,niliposhika nikakuta ni mshale ndipo nikapiga kelele kuomba msaada”alisema Mayala.
Kuhusu chanzo cha tukio hilo alisema ni kutokana na masuala ya kisiasa kwa kuwa siku hiyo kwenye mkutano huo kulitokea vurugu kubwa zilizosababishwa na wafuasi wa vyama vingine.
MTANZANIA
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe kamwe hawezi kukurupuka kulifufua Shirika la Ndege nchini ATC kwani uzembe na ubadhirifu uliofanywa unatia aibu hata kuzungumzia hadharani.
Mwakyembe alisema awali Shirika hilo lilikua na ndege 13 lakini sasa lina ndege moja tu.
“Shirika letu la ndege limekua na matukio mengi na mengine yanatia aibu hata kuyazungumzia hadharani,mtu analipia ndege ambayo ni mbovu haina hata matairi anasema ni ya ATCL
“Tumekua na mikataba ya kipuuzi ya kulaliwa tu,yaani mtu analaliwa kuanzia asubuhi hadi jioni.
Alisema kwa miaka miwili sasa wamekua wakihakiki madeni ya Shirika hilo ambayo ni zaidi ya bilioni140 pamoja na kujadiliana na wadai.
MTANZANIA
Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Rished Bade amesema hatishwi na kauli ya Mmiliki wa IPTL Herbinder Seth ya kutaka akamatwe na kufikishwa mahakamani.
Kauli ya kamishna Bade imekuja siku chache baada ya kampuni ya PAP na IPTL kuitaka bodi ya rufani ya kodi nchini iamuru kamishna mkuu wa TRA akamatwe na kupelekwa mahakamani kwa hatua yake ya kufuta hati ya uthibiti ulipaji wa kodiwa kampuni hiyo katika ununuzi wa hisa za IPTL.
Bade alisema siku zote mamlaka yake haimwonei mtu juu ya ulipwaji wa kodi.
“Sitishwi na mtu,tunatekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria zilizopo,kama ni singasinga unayemsemea mimi sijui unamaanisha nani”kama ni yule wa IPTLnajua ni mlipa kodi wangu,lazima alipe tu”alisema Bade.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook