Show ya Jahazi iliyoruka siku ya jana December 10 kulikuwa na ugeni kutoka Shirika la Utangazaji Uingereza BBC ambapo Mtangazaji Salim Kikeke alikuwepo kwa ajili ya mahojiano kwenye kipindi hicho.
Aliaanza kwa kuelezea kuhusu namna ambavyo BBC wanapata habari kutoka maeneo mbalimbali duniani; “Shirika la Utangazaji la BBC kimataifa ndio lenye waandishi wa habari wengi zaidi Duniani kuliko shirika lolote la habari la Kimataifa.. Kitu kikitokea kokote Duniani lazima hiyo taarifa tutakuwa nayo…”– Salim Kikeke.
Kikeke ameelezea namna ambavyo BBC wanaandaa habari; “Unavyojitayarisha nusu saa kabla ya kwenda hewani huwa tunafanya rehearsal jambo ambalo nakumbuka wakati tuko hapa Tanzania tulikuwa hatulifanyi na hata ukiwaambia watu wanasema kwanini ufanye rehearsal wakati umeshazoea…”
Mtangazaji huyo alitoa pongezi kwa kituo cha Clouds FM kutimiza miaka 15; “Nilitaka kutoa pongezi sana za kufikisha miaka 15 ya Clouds kutoa burudani na habari… Inanikumbusha mbali sana kwa sababu wakati Clouds inaanza tukiwa mtaani bado tunasikia kwamba jamani kuna redio mpya inakuja na ilikuwa kati ya redio za mwanzo mwanzo kabisa za FM…”– Salim Kikeke.
Hapa alizungumza kuhusu kitu kinapaswa kuzingatiwa zaidi kwenye uandishi wa habari; “Kinachozingatiwa zaidi ni misingi ya uandishi wa habari na ndiyo ya kuifuatilia kwa umakini.. Kama kuna taarifa imetoka na unaibeba hivyo hivyo bila ya kuithibitisha na bila ya kuitafuta upande wa pili unasemaje kuhusu taarifa hiyo… hicho ni cha kuzingatia kwa mwandishi wa habari yoyote… Kitu ambacho tunajisahahu ni kutokusoma, hatusomi kwa makini kufuatilia… Ukijitahidi kusoma kila kinachowezekana unakuwa taarifa unaifahamu…”– Kikeke.
Akiisimulia safari yake ya kwanza kufika Uingereza kwa ajili ya kuanza kazi na BBC, Kikeke amesema; “Nilipofika London, Tido Mhando ndio alikuwa Mkurugenzi pale, nilipofikia kwenye Hotel akanipigia simu na kusema kama nimewasili kesho niende kazini…“
Kuhusu malengo ya Dira ya Dunia, Kikeke amesema; “Katika zile wiki mbili za mwanzo ambazo nimekaa Tanzania nimeshafanya stori mbili… Nilienda Pemba.. Dira ya Dunia tulipoanza tulisema pamoja na kuwa tutakuwa tukiyataja kwa kuwa kama kuna vita unasema.. Sisi tumeweka ahadi kwamba tutatangaza habari nzuri ambazo zipo katika maeneo yetu…”
Hapa nimekuwekea Interview yote, unaweza kuisikiliza.
https://soundcloud.com/newstza-millardayo-com/kikeke-on-clouds-dec11
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook