Moja ya changamoto kubwa ya wanayokutana nayo waandishi wa Habari ni hii ambayo wanajikuta wakifanya kazi katika mazingira magumu, ikiwemo matukio ya kupigwa na nyinginezo.
Mwandishi wa Habari wa kituo cha Telemundo, Andres Herrera alivamiwa na kupigwa na mtu mmoja California, Marekani wakati akiendelea na majukumu yake mtaani.
Jamaa huyo alimuuliza Herrera kama anafanya kazi ya uandishi wa habari, alipomjibu ‘ndiyo’ jamaa alimsogelea na kuanza kumpiga.
Polisi wamesema jamaa ambaye amefanya kosa hilo tayari ana mashtaka mengine ambayo anakabiliwa nayo yakimhusisha na matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
https://www.youtube.com/watch?v=arbOlBMtjE0
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook