Kuna hiki ambacho alinukuliwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuhusu msimamo wake na michoro ya sticker kwenye gari; “Sioni lolote baya na kutiwa michoro kwenye matatu. Twahitajika kuunga mkono vijana wetu kufanikisha biashara yao, mradi michoro hiyo haitazuia dereva kuona njia vizuri”
Hayo aliyasema mwaka jana wakati alipokuwa akizindua mfumo mpya wa kielektroniki wa kulipia nauli, taarifa zilizonifikia jana ni juu ya magari ya abiria maarufu kama matatu zenye michoro hiyo, ikiwemo moja yenye mchoro wa picha ya Rais Kenyatta kukamatwa na polisi Kenya baada ya kufanyika msako.
Matatu zilizokamatwa zipo zenye picha ya Gavana wa Mombasa, Hassan Joho na nyingine yenye nembo ya taifa, muda mfupi baadaye moja ya matatu hizo iliachiwa baada ya kuondoa michoro hiyo.
Wamiliki wa matatu hizo wamelalamika kwamba Rais aliruhusu michoro hiyo kuokoa ajira za vijana na ndio maana wengine waliamua kuweka picha za rais huyo kama njia ya kusheherekea uongozi wake.
Mkuu wa trafiki eneo la Pwani mwa Kenya, Martin Kariuki anasema kuwa hakujafanyika mabadiliko yeyote kwenye sheria ya trafiki kuruhusu matumizi ya picha za namna hiyo kwenye magari hivyo bado ni kosa kisheria kuweka picha hizo katika gari za abiria.
Nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter InstaFacebook