Rais wa Fc Barcelona Joseph Bartomeu anatarajiwa kumfukuza kazi kocha wa klabu hiyo Luis Enrique baada ya mchezo wa ligi ya Hispania utakaopigwa jumapili dhidi ya mabingwa watetezi Atletico Madrid baada ya uhusiano wake na Lionel Messi kuendelea kuwa mbaya .
Taarifa zaidi zinadai kuwa rais huyo wa Barcelona alikutana na Messi hapo jana (ijumaa) na kumuarifu kuhusu mpango wake na inaaminika kuwa Messi aliunga mkono mpango huo huku akitoa maoni ya nani anapswa kuwa mrithi wa Enrique mara atakapofukuzwa.
Messi ameomba kurejeshwa kwa kocha wake wa zamani Mdachi Frank Rijkaard ambaye ndiye alikuwa kocha wa kwanza kumtoa Messi wakati akiwa kwenye kikosi cha timu za vijana na kumpa mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya wakubwa kabla ya kuingia na kufikia mahali aliko leo hii.
Uhusiano wa Messi na kocha wake umeendelea kuripotiwa kuwa hauko vizuri pamoja na ushindi ilioupata Barcelona katika mchezo wake dhidi ya Elche ambako ilishinda kwa mabao matano huku Messi akishangiliwa na mashabiki wa Barcelona na wengine wakimzomea kocha .
Hivi karibuni hali imeendelea kuwa mbaya ndani ya Barcelona baada ya kufukuzwa kazi kwa Andoni Zubizaretta ambaye ni mkurugenzi wa ufundi huku msaidizi wake Carles Puyol naye akiamua kuachia ngazi.