Wakati saa zikizidi kupungua kuelekea kwenye uteguzi wa kitendawili cha nani atatangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2014 katika tuzo za Ballo D’or zinazotolewa huko Uswisi hali ya kuchanganyikiwa kwa tuzo hizo imewakumba karibu wapenzi wote wa soka.
Kinyang’anyiro hicho kikiwa kinawajumuisha wachezaji watatu ambao ni Manuel Neur, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kimesababisha ubishani mwingi mitaani na kwenye mitandao ya kijamii japo kura za wengi zimeelekea kuegemea kwa mchezaji mmoja kati ya watatu hao.
Ubishi huu na ile hali ya kutoweza kufahamu mapema mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kumehamia mpaka kwenye vyombo vya habari ambako jarida moja maarufu la mchezo wa soka nchini Ufaransa limeandaa cover tatu tofauti ambayo yana picha za wachezaji watatu wanaowania tuzo hizo huku wakichapisha cover lenye picha ya yule atakayeshinda tuzo hiyo kwa toleo lao la kesho.
Wahariri wa jarida hili la France Football wamekwenda mbali zaidi ambapo ndnai ya machapisho haya matatu kila moja lina tahariri tofauti ikimhusu yule ambaye atashinda tuzo hii usiku wa leo.
Hadi sasa kura za wengi zimemuelekea Cristiano Ronaldo na hali inavyoonekana inaelekea atatangazwa kuwa mshindi kwa mara yake ya pili mfululizo na hii inamaanisha kuwa picha yake ndio itakayoonekana kwenye chapisho la kesho la France Football.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook