Siku ya jana January 12 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha alikuwa katika mahojiano kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV, hapa kuna kile alichokizungumza kuhusu ishu ya nini kifanywe kuwabana wakwepa kodi na wala rushwa, msimamo wake kugombea Urais 2015 na ishu ya wahusika waliochukua Fedha za Escrow.
“Kwa nchi yetu, upande mmoja wa hili la kukwepa kodi na upande wa rushwa ukitaka kukomesha na lenyewe linasubiria Katiba Mpya tutakapokwenda kwenye Sheria hili tutasimamia mpaka koo litakauka… Yaani mtu kupokea rushwa anatakiwa anatakiwa akikadiria hivi siku nikipokea rushwa nikikamatwa madhara yake ni nini…“– Mwigulu Nchemba.
Anatakiwa ajue siku ileile kwamba hakuna dhamana, taratibu za kimahakama zitaendelea akiwa ndani nakutoka hapo adhabu yake inatakiwa imtishe… Kama mtu amesababisha hasara ya bilioni thelathini, kama adhabu nii kumuondoa tu kwenye nafasi aliyokuwa nayo umempa likizo akatumie fedha… Umempa send-off akasherekee fedha ya umma…”– Mwigulu Nchemba.
Kuhusu hatua ambazo zimefikiwa mpaka sasa kwa wale waliochukua pesa za Escrow, Naibu Waziri huyo alisema; “Taarifa nilizonazo tayari Mamlaka ya Mapato imeshafanya hesabu… Kuhusu haya mambo ya Kodi kweli tumedhamiria, kwamba lazima kodi ilipwe na hili si jambo la mjadala… Hatuwezi tukasamehe kodi kubwa vile halafu tukakimbizana na mama anayeuza mchicha…”– Mwigulu Nchemba.
Alipoulizwa kuhusu msimamo wake kwenye Uchaguzi 2015 alijibu; “Ninataka nifocus sana kumsaidia Waziri kwenye haya majukumu ambayo tumepewa na Mheshimiwa Rais kuhakikisha kwamba Serikali inatimiza wajibu wake… Nikirudi kwenye Chama namsaidia Katibu Mkuu kusimamia misingi ya Chama… Nisingependa niwe miongoni mwa wanaovunja miiko.. Tutavuka mto tukishafika mtoni kufuatana na taratibu zetu…”– Mwigulu Nchemba.
Msimamo wangu kwenye masuala ya msingi yanayohusu taifa letu huwa hauyumbi wanaonifahamu wanajua…”
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook